Mtu mmoja akamwambia Daudi ya kwamba, Ahithofeli yu katika hao waliopatana na Absalomu; Daudi akasema, Ee BWANA, nakusihi, uugeuze ushauri wa Ahithofeli uwe ubatili.
Yobu 12:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Yeye huwaondoa washauri wakiwa wamevuliwa nguo, Naye huwafanya waamuzi kuwa ni wapumbavu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huwaacha washauri waende zao uchi, huwafanya waamuzi kuwa wapumbavu. Biblia Habari Njema - BHND Huwaacha washauri waende zao uchi, huwafanya waamuzi kuwa wapumbavu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huwaacha washauri waende zao uchi, huwafanya waamuzi kuwa wapumbavu. Neno: Bibilia Takatifu Yeye huwaondoa washauri wakiwa wametekwa nyara, naye huwapumbaza wanaotoa maamuzi. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye huwaondoa washauri wakiwa wametekwa nyara, naye huwapumbaza wanaotoa maamuzi. BIBLIA KISWAHILI Yeye huwaondoa washauri wakiwa wamevuliwa nguo, Naye huwafanya waamuzi kuwa ni wapumbavu. |
Mtu mmoja akamwambia Daudi ya kwamba, Ahithofeli yu katika hao waliopatana na Absalomu; Daudi akasema, Ee BWANA, nakusihi, uugeuze ushauri wa Ahithofeli uwe ubatili.
Naye Absalomu na watu wote wa Israeli wakasema, Ushauri wa Hushai, Mwarki, ni mwema kuliko ushauri wa Ahithofeli. Kwa maana BWANA alikuwa amekusudia kuuvunja ushauri mwema wa Ahithofeli, ili BWANA alete mabaya juu ya Absalomu.
Naye Ahithofeli alipoona ya kuwa ushauri wake haukufuatwa, akatandika punda wake, akaondoka, akaenda nyumbani kwake, mjini mwake, akaitengeneza nyumba yake, akajinyonga; akafa, akazikwa kaburini mwa babaye.
Dunia imetiwa mkononi mwa waovu; Yeye hufunika nyuso za waamuzi wake; Kama si yeye, ni nani basi?
kwa sababu hiyo mimi nitafanya tena kazi ya ajabu kati ya watu hawa, kazi ya ajabu na mwujiza; na akili za watu wao wenye akili zitapotea, na ufahamu wa wenye busara wao utafichwa.
Naye ameyathibitisha maneno yake, aliyoyanena juu yetu, na juu ya waamuzi wetu waliotuamua, kwa kumletea mambo maovu makuu; maana chini ya mbingu zote halikutendeka jambo kama hili, lilivyotendeka juu ya Yerusalemu.