Lakini Mungu je! Yamkini atakaa na watu duniani? Tazama, mbingu na mbingu za mbingu za mbingu hazikutoshi; seuze nyumba hii niliyoijenga!
Yobu 11:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ni juu mno kama mbingu; waweza kufanya nini wewe? Ni wenye kina kuliko kuzimuni; waweza kujua nini wewe? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ukuu wake wapita mbingu, wewe waweza nini? Kimo chake chapita Kuzimu, wewe waweza kujua nini? Biblia Habari Njema - BHND Ukuu wake wapita mbingu, wewe waweza nini? Kimo chake chapita Kuzimu, wewe waweza kujua nini? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ukuu wake wapita mbingu, wewe waweza nini? Kimo chake chapita Kuzimu, wewe waweza kujua nini? Neno: Bibilia Takatifu Ni juu mno kuliko mbingu: unaweza kufanya nini? Kina chake ni kirefu kuliko Kuzimu: wewe unaweza kujua nini? Neno: Maandiko Matakatifu Ni juu mno kuliko mbingu: waweza kufanya nini? Kina chake ni kirefu kuliko kuzimu: wewe waweza kujua nini? BIBLIA KISWAHILI Ni juu mno kama mbingu; waweza kufanya nini wewe? Ni wenye kina kuliko kuzimuni; waweza kujua nini wewe? |
Lakini Mungu je! Yamkini atakaa na watu duniani? Tazama, mbingu na mbingu za mbingu za mbingu hazikutoshi; seuze nyumba hii niliyoijenga!
Yeye Mwenyezi hamwezi kumwona; Yeye ni mkuu mwenye uweza; Tena mwenye hukumu, na mwingi wa haki, hataonea.
Kama vile wingu likomavyo na kutoweka, Ndivyo alivyo huyo ashukaye kuzimuni, hatazuka tena kabisa.
Maana, kama mbingu zilivyoinuka juu ya nchi, Ndivyo fadhili zake zilivyo kuu kwa wamchao.
Na walisifu jina la BWANA, Maana jina lake peke yake limetukuka; Adhama yake i juu ya nchi na mbingu.
Haki yako ni kama milima ya Mungu, Hukumu zako ni vilindi vikuu, Ee BWANA, unawalinda wanadamu na wanyama.
Ni nani aliyepanda mbinguni na kushuka chini? Ni nani aliyekamata upepo kwa makonzi yake? Ni nani aliyeyafunga maji ndani ya nguo yake? Ni nani aliyefanya imara ncha zote za nchi? Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwanawe, kama wajua?
Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, ndivyo njia zangu zilivyo juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.
Wajapochimba waingie katika kuzimu, mkono wangu utawatoa huko; nao wajapopanda hata mbinguni, nitawateremsha toka huko.