Yobu 11:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Je! Wewe waweza kuuvumbua ukuu wa Mungu? Waweza kuufikia upeo wa huyo Mwenyezi? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Je, unaweza kugundua siri zake Mungu na kujua ukomo wake yeye Mungu mwenye nguvu? Biblia Habari Njema - BHND “Je, unaweza kugundua siri zake Mungu na kujua ukomo wake yeye Mungu mwenye nguvu? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Je, unaweza kugundua siri zake Mungu na kujua ukomo wake yeye Mungu mwenye nguvu? Neno: Bibilia Takatifu “Je, unaweza kujua siri za Mungu? Je, unaweza kuyachunguza mambo yote kumhusu Mwenyezi? Neno: Maandiko Matakatifu “Je, waweza kujua siri za Mungu? Je, waweza kuyachunguza mambo yote kumhusu Mwenyezi? BIBLIA KISWAHILI Je! Wewe waweza kuuvumbua ukuu wa Mungu? Waweza kuufikia upeo wa huyo Mwenyezi? |
Tazama, hivi ni viunga tu vya njia zake; Na jinsi yalivyo madogo manong'ono tusikiayo katika habari zake! Lakini ngurumo za uweza wake ni nani awezaye kuzielewa?
Tazama, nitakujibu, katika neno hili huna haki; Kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu.
Yeye Mwenyezi hamwezi kumwona; Yeye ni mkuu mwenye uweza; Tena mwenye hukumu, na mwingi wa haki, hataonea.
Mungu hunguruma kwa kustaajabisha kwa sauti yake; Hufanya mambo makuu, ambayo hatuwezi kuyaelewa.
Ni nani huyu afichaye ushauri bila maarifa? Kwa maana, nimesema maneno nisiyoyafahamu, Mambo ya ajabu ya kunishinda mimi, nisiyoyajua.
Njia yako ilikuwa katika bahari. Na mapito yako yalikuwa katika maji makuu; Hatua zako hazikujulikana.
Ni nani aliyepanda mbinguni na kushuka chini? Ni nani aliyekamata upepo kwa makonzi yake? Ni nani aliyeyafunga maji ndani ya nguo yake? Ni nani aliyefanya imara ncha zote za nchi? Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwanawe, kama wajua?
Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho.
Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.
Akasema, Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na yeyote ambaye Mwana apenda kumfunulia.
Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazieleweki!
Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.
Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.
Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nilipewa neema hii ya kuwahubiria Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;