Yobu 11:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini macho ya waovu yataingia kiwi, Nao hawatakuwa na njia ya kukimbilia, Na matumaini yao yatakuwa ni kutoa roho. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini waovu macho yao yatafifia, njia zote za kutorokea zitawapotea; tumaini lao la mwisho ni kukata roho!” Biblia Habari Njema - BHND Lakini waovu macho yao yatafifia, njia zote za kutorokea zitawapotea; tumaini lao la mwisho ni kukata roho!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini waovu macho yao yatafifia, njia zote za kutorokea zitawapotea; tumaini lao la mwisho ni kukata roho!” Neno: Bibilia Takatifu Bali macho ya waovu hayataona, wokovu utawaepuka; tarajio lao litakuwa ni hangaiko la mtu anayekata roho.” Neno: Maandiko Matakatifu Bali macho ya waovu hayataona, wokovu utawaepuka; tarajio lao litakuwa ni hangaiko la mtu anayekata roho.” BIBLIA KISWAHILI Lakini macho ya waovu yataingia kiwi, Nao hawatakuwa na njia ya kukimbilia, Na matumaini yao yatakuwa ni kutoa roho. |
Atang'olewa katika hema yake aliyokuwa akiitumaini; Naye atapelekwa kwake mfalme wa vitisho.
Maana tumaini la mpotovu ni nini, ingawa ajipatia faida, Hapo Mungu amwondoleapo roho yake?
Ambao wangojea mauti, lakini hawayapati; Na kuyachimbulia kuliko watafutavyo hazina iliyostirika;
Kwamba Mungu angekuwa radhi kuniponda; Kwamba angeulegeza mkono wake na kunikatilia mbali!
Utazame mkono wangu wa kulia ukaone, Kwa maana sina mtu anijuaye. Makimbilio yamenipotea, Hakuna wa kunitunza roho.
Nimechoka kwa kulia kwangu, Koo yangu imekauka. Macho yangu yamedhoofika Kwa kumngoja Mungu wangu.
Nao wachungaji watakuwa hawana njia ya kukimbia, wala walio hodari katika kundi hawataokoka.
Macho yetu yamechoka Kwa kuutazamia bure msaada wetu; Katika kungoja kwetu tumengojea taifa Lisiloweza kutuokoa.
mimi nami nitawatenda jambo hili; nitaamrisha uje juu yenu utisho, hata kifua kikuu na homa, zitakazoharibu macho yenu, na kuidhoofisha roho; nanyi mtapanda mbegu yenu bure, kwa kuwa adui zenu wataila.
Naye apigaye mbio atapotewa na kimbilio; Wala aliye hodari hataongeza nguvu zake; Wala shujaa hatajiokoa nafsi yake;
Wala katika mataifa hayo hutapata raha iwayo yote, wala hutakuwa na kituo cha wayo wa mguu wako; lakini BWANA atakupa huko moyo wa kutetema, na macho ya kuzimia, na roho ya kudhoofika;
sisi je! Tutapataje kupona, tukipuuza wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliomsikia;