Yobu 11:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wewe ukiuweka moyo wako kwa uelekevu, Na kumnyoshea mikono yako; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Yobu, ukiufanya moyo wako mnyofu, utainua mikono yako kumwomba Mungu! Biblia Habari Njema - BHND “Yobu, ukiufanya moyo wako mnyofu, utainua mikono yako kumwomba Mungu! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Yobu, ukiufanya moyo wako mnyofu, utainua mikono yako kumwomba Mungu! Neno: Bibilia Takatifu “Hata sasa ukiutoa moyo wako kwake na kumwinulia mikono yako, Neno: Maandiko Matakatifu “Hata sasa ukiutoa moyo wako kwake na kumwinulia mikono yako, BIBLIA KISWAHILI Wewe ukiuweka moyo wako kwa uelekevu, Na kumnyoshea mikono yako; |
Walakini, yameonekana kiasi cha mema ndani yako, kwa kuwa umeyaondoa Maashera katika nchi, na moyo wako umeukaza kumtafuta Mungu.
Tazama, yu heri mtu yule Mungu amwadhibuye; Kwa hiyo usidharau kurudiwa na huyo Mwenyezi.
Katika siku ya taabu yangu nilimtafuta Bwana; Mkono wangu ulinyoshwa usiku, bila kulegea; Nafsi yangu ilikataa kufarijika.
Naam, wasiwe kama baba zao, Kizazi cha ukaidi na uasi. Kizazi kisichojitengeneza moyo, Wala roho yake haikuwa amini kwa Mungu.
Jicho langu limefifia kwa ajili ya mateso BWANA, ninakuita kila siku; Ninakunyoshea Wewe mikono yangu.
Musa akamwambia, Mara nitakapotoka mjini nitamwinulia BWANA mikono yangu; na hizo ngurumo zitakoma, wala haitanyesha mvua ya mawe tena; ili upate kujua ya kuwa dunia hii ni ya BWANA.
Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana.
Basi Samweli akawaambia nyumba yote ya Israeli, akasema, Ikiwa mnamrudia BWANA kwa mioyo yenu yote, basi, iondoleeni mbali miungu migeni, nayo Maashtorethi yatoke kwenu, mkamwelekezee BWANA mioyo yenu, mkamtumikie yeye peke yake; naye atawaokoa katika mikono ya Wafilisti.