Yobu 11:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa kuwa yeye awajua watu baradhuli; Anapouona uovu, je; hatauangalia? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mungu anajua watu wasiofaa; akiona maovu yeye huchukua hatua. Biblia Habari Njema - BHND Mungu anajua watu wasiofaa; akiona maovu yeye huchukua hatua. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mungu anajua watu wasiofaa; akiona maovu yeye huchukua hatua. Neno: Bibilia Takatifu Hakika anawatambua watu wadanganyifu; naye aonapo uovu, je, haangalii? Neno: Maandiko Matakatifu Hakika anawatambua watu wadanganyifu; naye aonapo uovu, je, haangalii? BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa yeye awajua watu baradhuli; Anapouona uovu, je; hatauangalia? |
Umeona, maana unaangalia matatizo na dhiki, Uyatwae mkononi mwako. Mtu duni hukuachia nafsi yake, Maana umekuwa msaidizi wa yatima.
Ujapokuwa unaona maskini kuonewa, na hukumu na haki kuondolewa kwa jeuri katika jimbo, usilistaajabie jambo hilo; kwa sababu, Aliye Juu kuliko walio juu huangalia; Tena wako walio juu kupita hao.
Wala hawafikiri mioyoni mwao ya kwamba naukumbuka uovu wao wote; sasa matendo yao wenyewe yamewazunguka pande zote; yako mbele za uso wangu.
Wewe uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu, wewe usiyeweza kutazama ukaidi, mbona unawaangalia watendao kwa hila; na kunyamaza kimya, hapo mtu mwovu ammezapo mtu aliye mwenye haki kuliko yeye;
Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, maana vitu vyote ni tupu na kuwekwa wazi machoni pake yeye ambaye tunapaswa kuwajibika kwake.
nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye fikira na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.