Mimi nikiwa mwovu, ole wangu! Nami nikiwa mwenye haki, walakini sitainua kichwa changu; Maana nimejaa aibu Nikiyaangalia mateso yangu.
Yobu 10:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ujapojua ya kuwa mimi si mwovu; Wala hapana awezaye kuokoa kutoka kwa mkono wako? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wewe wajua kwamba mimi sina hatia, na hakuna wa kuniokoa mikononi mwako. Biblia Habari Njema - BHND Wewe wajua kwamba mimi sina hatia, na hakuna wa kuniokoa mikononi mwako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wewe wajua kwamba mimi sina hatia, na hakuna wa kuniokoa mikononi mwako. Neno: Bibilia Takatifu ingawa unajua kuwa mimi sina hatia, na hakuna awezaye kunitoa mkononi mwako? Neno: Maandiko Matakatifu ingawa wajua kuwa mimi sina hatia, na hakuna awezaye kunitoa mkononi mwako? BIBLIA KISWAHILI Ujapojua ya kuwa mimi si mwovu; Wala hapana awezaye kuokoa kutoka katika mkono wako? |
Mimi nikiwa mwovu, ole wangu! Nami nikiwa mwenye haki, walakini sitainua kichwa changu; Maana nimejaa aibu Nikiyaangalia mateso yangu.
Laiti ningekuwa na mtu wa kunisikia! (Tazama, sahihi yangu ni hii, Mwenyezi na anijibu); Laiti ningekuwa na hayo mashitaka yaliyoandikwa na adui yangu!
Basi hao watu watatu wakaacha kumjibu Ayubu, kwa sababu alikuwa mwenye haki machoni pake mwenyewe.
Basi ikawa, baada ya BWANA kumwambia Ayubu maneno hayo, BWANA akamwambia huyo Elifazi Mtemani, Hasira zangu zinawaka juu yako, na juu ya hao rafiki zako wawili; kwa kuwa ninyi hamkunena yaliyo sawa katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu.
Umenijaribu moyo wangu, umenijia usiku, Umenichunguza usione neno; Nimenuia kinywa changu kisikose,
Naam, tangu siku ya leo, mimi ndiye; wala hakuna awezaye kuokoa katika mkono wangu; mimi nitatenda kazi, naye ni nani awezaye kuizuia?
Basi sasa, kama mkiwa tayari wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zumari, na namna zote za ngoma, kuanguka na kuisujudia sanamu niliyoisimamisha, ni vema; bali msipoisujudia, mtatupwa saa iyo hiyo katika tanuri liwakalo moto; naye ni nani Mungu yule atakayewaokoa ninyi mikononi mwangu?
Na sasa nitaifunua aibu yake mbele ya macho ya wapenzi wake, wala hapana mtu atakayemwokoa katika mkono wangu.
Maana mimi nitakuwa kama simba kwa Efraimu, na kama mwanasimba kwa nyumba ya Yuda; mimi, naam, mimi nitararua, kisha nitakwenda zangu; nitachukua mbali, wala hapatakuwa na mtu wa kuokoa.
Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo wangu.
Kwa maana kujisifu kwetu ni huku, ushuhuda wa dhamiri yetu, ya kwamba kwa utakatifu na weupe wa moyo utokao kwa Mungu; si kwa hekima ya mwili, bali kwa neema ya Mungu; tulienenda katika dunia, na hasa kwenu ninyi.
Fahamu sasa ya kuwa Mimi, naam, Mimi ndiye, Wala hapana Mungu mwingine ila Mimi; Naua Mimi, nahuisha Mimi, Nimejeruhi, tena naponya; Wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu,
Ninyi ni mashahidi, na Mungu pia, jinsi tulivyokaa kwenu ninyi mnaoamini, kwa utakatifu, na kwa haki, bila kulaumiwa;
Mungu, Mungu BWANA, naam, Mungu, Mungu BWANA, yeye anajua, na Israeli naye atajua; kama ni katika uasi, au kama ni katika kosa juu ya BWANA, usituokoe hivi leo;