Yobu 10:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kichwa changu kikijiinua, waniwinda kama simba; Tena wajionesha kwangu kuwa wa ajabu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nikiinua kichwa tu waniwinda kama simba na kuniponda tena kwa maajabu yako. Biblia Habari Njema - BHND Nikiinua kichwa tu waniwinda kama simba na kuniponda tena kwa maajabu yako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nikiinua kichwa tu waniwinda kama simba na kuniponda tena kwa maajabu yako. Neno: Bibilia Takatifu Nikiinua kichwa changu juu, unaniwinda kama simba, na kuonesha tena uwezo wa kutisha dhidi yangu. Neno: Maandiko Matakatifu Kama nikiinua kichwa changu juu, unaninyatia kama simba, na kuonyesha tena uwezo wa kutisha dhidi yangu. BIBLIA KISWAHILI Kichwa changu kikijiinua, waniwinda kama simba; Tena wajionesha kwangu kuwa wa ajabu. |
Amenirarua katika ghadhabu zake, na kunionea; Amesagasaga meno juu yangu; Mtesi wangu hunikazia macho makali.
Nilijituliza hata asubuhi; kama simba, anaivunja mifupa yangu yote; Tangu mchana hata usiku wanimaliza.
Basi, kwa hiyo, simba atokaye mwituni atawaua, mbwamwitu wa jioni atawateka, chui ataivizia miji yao, kila mtu atokaye humo atararuliwa vipande vipande; kwa sababu makosa yao ni mengi, na kurudi nyuma kwao kumezidi.
Maana mimi nitakuwa kama simba kwa Efraimu, na kama mwanasimba kwa nyumba ya Yuda; mimi, naam, mimi nitararua, kisha nitakwenda zangu; nitachukua mbali, wala hapatakuwa na mtu wa kuokoa.
Simba amekwisha kunguruma, ni nani asiyeogopa? Bwana MUNGU amenena, ni nani awezaye neno ila kutabiri?
ndipo atakapofanya BWANA mapigo yako yawe ya ajabu, na mapigo ya uzao wako, mapigo makubwa kwa kweli, ya kudumu sana, na magonjwa mazito ya kudumu sana.