Akusanyaye wakati wa joto ni mwana mwenye hekima; Bali asinziaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha.
Yeremia 8:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mavuno yamepita, wakati wa joto umekwisha, wala sisi hatukuokoka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Mavuno yamepita, kiangazi kimekwisha, nasi bado hatujaokolewa! Biblia Habari Njema - BHND “Mavuno yamepita, kiangazi kimekwisha, nasi bado hatujaokolewa! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Mavuno yamepita, kiangazi kimekwisha, nasi bado hatujaokolewa! Neno: Bibilia Takatifu “Mavuno yamepita, kiangazi kimekwisha, nasi hatujaokolewa.” Neno: Maandiko Matakatifu “Mavuno yamepita, kiangazi kimekwisha, nasi hatujaokolewa.” BIBLIA KISWAHILI Mavuno yamepita, wakati wa joto umekwisha, wala sisi hatukuokoka. |
Akusanyaye wakati wa joto ni mwana mwenye hekima; Bali asinziaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha.
Tazama, sauti ya kilio cha binti ya watu wangu, itokayo katika nchi iliyo mbali sana; Je! BWANA hayumo katika Sayuni? Mfalme wake hayumo ndani yake? Mbona wamenikasirisha kwa sanamu zao walizochonga, na kwa ubatili wa kigeni?
Kwa sababu ya maumivu ya binti ya watu wangu nimeumia mimi; nimevaa kaniki; ushangao umenishika.
Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;
watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiwa kwako.