Naye BWANA akatuma juu yake vikosi vya Wakaldayo, na vikosi vya Washami, na vikosi vya Wamoabi, na vikosi vya wana wa Amoni, akawatuma juu ya Yuda ili kuiharibu, sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa mkono wa watumishi wake manabii.
Yeremia 6:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wachungaji na makundi yao ya kondoo watamjia; watapiga hema zao karibu naye pande zote; watalisha kila mmoja mahali pake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wataujia kama wachungaji na makundi yao, watapiga hema zao kuuzunguka kila mmoja sehemu yake, wapate kuyaongoza makundi yao. Biblia Habari Njema - BHND Watu wataujia kama wachungaji na makundi yao, watapiga hema zao kuuzunguka kila mmoja sehemu yake, wapate kuyaongoza makundi yao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wataujia kama wachungaji na makundi yao, watapiga hema zao kuuzunguka kila mmoja sehemu yake, wapate kuyaongoza makundi yao. Neno: Bibilia Takatifu Wachungaji pamoja na makundi yao watakuja dhidi yake; watapiga mahema yao kumzunguka, kila mmoja akichunga kundi lake mwenyewe.” Neno: Maandiko Matakatifu Wachungaji pamoja na makundi yao watakuja dhidi yake; watapiga mahema yao kumzunguka, kila mmoja akichunga kundi lake mwenyewe.” BIBLIA KISWAHILI Wachungaji na makundi yao ya kondoo watamjia; watapiga hema zao karibu naye pande zote; watalisha kila mmoja mahali pake. |
Naye BWANA akatuma juu yake vikosi vya Wakaldayo, na vikosi vya Washami, na vikosi vya Wamoabi, na vikosi vya wana wa Amoni, akawatuma juu ya Yuda ili kuiharibu, sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa mkono wa watumishi wake manabii.
Wachungaji wengi wameliharibu shamba langu la mizabibu, wamelikanyaga fungu langu chini ya miguu yao, wamefanya fungu langu zuri kuwa jangwa la ukiwa.
Wachungaji wako wanalala usingizi, Ee mfalme wa Ashuru; watu wako wenye heshima wamepumzika; watu wako wametawanyika juu ya milima, wala hapana mtu wa kuwakusanya.
Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote;