Moyo wangu unamlilia Moabu; wakuu wake wanakimbilia Soari kama ndama wa miaka mitatu; kwa maana wanapanda mbavu za Luhithi wakilia; maana katika njia iendayo hata Horonaimu wanatoa kilio cha maangamizi.
Yeremia 51:54 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Sauti ya kilio kutoka Babeli, Na ya uangamizi mkuu toka nchi ya Wakaldayo! Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Sikiliza! Kilio kinasikika kutoka Babuloni! Kishindo cha maangamizi makubwa kutoka nchi ya Wakaldayo! Biblia Habari Njema - BHND “Sikiliza! Kilio kinasikika kutoka Babuloni! Kishindo cha maangamizi makubwa kutoka nchi ya Wakaldayo! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Sikiliza! Kilio kinasikika kutoka Babuloni! Kishindo cha maangamizi makubwa kutoka nchi ya Wakaldayo! Neno: Bibilia Takatifu “Sauti ya kilio inasikika kutoka Babeli, sauti ya uharibifu mkuu kutoka nchi ya Wakaldayo. Neno: Maandiko Matakatifu “Sauti ya kilio inasikika kutoka Babeli, sauti ya uharibifu mkuu kutoka nchi ya Wakaldayo. BIBLIA KISWAHILI Sauti ya kilio kutoka Babeli, Na ya uangamizi mkuu toka nchi ya Wakaldayo! |
Moyo wangu unamlilia Moabu; wakuu wake wanakimbilia Soari kama ndama wa miaka mitatu; kwa maana wanapanda mbavu za Luhithi wakilia; maana katika njia iendayo hata Horonaimu wanatoa kilio cha maangamizi.
Kama vile joto katika mahali pakavu Utaushusha mshindo wa wageni; Kama ilivyo joto kwa kivuli cha wingu, Wimbo wa hao watishao utashushwa.
Wachinjeni mafahali wake wote; Na wateremkie machinjoni; Ole wao! Maana siku yao imewadia, Wakati wa kujiliwa kwao.
Mfalme wa Babeli amesikia habari zao, Na mikono yake imekuwa dhaifu; Dhiki imemshika, na maumivu, Kama ya mwanamke akiwa katika uchungu wa kujifungua.
Kwa kishindo cha kutwaliwa Babeli nchi itatetemeka, Na kilio chake chasikiwa katika mataifa.
Na katika siku ile, asema BWANA kutakuwako sauti ya kilio kutoka lango la samaki, na mlio mkuu katika mtaa wa pili, na mshindo mkuu kutoka milimani.