Yeremia 51:48 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ndipo mbingu, na nchi, na vitu vyote vilivyomo, vitaimba kwa furaha juu ya Babeli; kwa maana watu waangamizao watamjia kutoka kaskazini, asema BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha mbingu, dunia na vyote vilivyomo vitaimba kwa furaha kuhusu kuanguka kwa Babuloni, waangamizi watakapofika kutoka kaskazini kuushambulia. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.” Biblia Habari Njema - BHND Kisha mbingu, dunia na vyote vilivyomo vitaimba kwa furaha kuhusu kuanguka kwa Babuloni, waangamizi watakapofika kutoka kaskazini kuushambulia. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha mbingu, dunia na vyote vilivyomo vitaimba kwa furaha kuhusu kuanguka kwa Babuloni, waangamizi watakapofika kutoka kaskazini kuushambulia. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.” Neno: Bibilia Takatifu Ndipo mbingu na dunia na vyote vilivyomo vitapiga kelele za shangwe juu ya Babeli, kwa kuwa kutoka kaskazini waangamizi watamshambulia,” asema Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo mbingu na dunia na vyote vilivyomo ndani yake vitapiga kelele za shangwe juu ya Babeli, kwa kuwa kutoka kaskazini waharabu watamshambulia,” asema bwana. BIBLIA KISWAHILI Ndipo mbingu, na nchi, na vitu vyote vilivyomo, vitaimba kwa furaha juu ya Babeli; kwa maana watu waangamizao watamjia kutoka kaskazini, asema BWANA. |
Imbeni, enyi mbingu, maana BWANA ametenda hayo; Pigeni kelele, enyi mabonde ya nchi; Pazeni nyimbo, enyi milima; Nawe, msitu, na kila mti ndani yake. Maana BWANA amemkomboa Yakobo, Naye atajitukuza katika Israeli.
Haya, tokeni katika Babeli, Kimbieni kutoka kwa Wakaldayo; Hubirini kwa sauti ya kuimba, tangazeni haya, Yatamkeni mpaka mwisho wa dunia, semeni, BWANA amemkomboa mtumishi wake, Yakobo.
Imbeni, enyi mbingu; ufurahi, Ee nchi; Pazeni sauti ya kuimba, enyi milima; Kwa kuwa BWANA amewafariji watu wake, Naye atawahurumia watu wake walioteswa.
Maana toka kaskazini taifa linakuja juu yake, litakaloifanya nchi yake kuwa ukiwa; wala hakuna mtu atakayekaa humo; wamekimbia, wamekwenda zao, mwanadamu na mnyama pia.
Angalia, watu wanakuja watokao kaskazini; na taifa kubwa, na wafalme wengi wataamshwa toka pande za mwisho za dunia.
Kwa maana juu ya Babeli nitaamsha na kuleta kusanyiko la mataifa makubwa, toka nchi ya kaskazini; nao watajipanga juu yake; kutoka huko atatwaliwa; mishale yao itakuwa kama ya mtu shujaa aliye stadi; hakuna hata mmoja utakaorudi bure.
Kwa maana mwenye kuangamiza amefika kwake; Naam, amefika Babeli; Na mashujaa wake wametwaliwa; Pinde zao zimevunjika kabisa; Maana BWANA ni Mungu wa kisasi; Hakika yake yeye atalipa.
Furahini juu yake, enyi mbingu, na enyi watakatifu, mitume na manabii; kwa maana Mungu ametoa hukumu kwa ajili yenu juu yake.