Na, tazama, linakuja kundi la watu, wapanda farasi, wakienda wawili wawili. Akajibu na kusema, Babeli umeanguka, umeanguka; na sanamu zote za miungu yake zimevunjwa chini.
Yeremia 51:47 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi angalia, siku zitakuja, ambazo katika siku hizo, nitafanya hukumu juu ya sanamu za Babeli, na nchi yake yote itatahayarika; na watu wake wote waliouawa wataanguka katikati yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kweli siku zaja, nitakapoadhibu sanamu za Babuloni; nchi yake yote itatiwa aibu, watu wake wote watauawa humohumo. Biblia Habari Njema - BHND Kweli siku zaja, nitakapoadhibu sanamu za Babuloni; nchi yake yote itatiwa aibu, watu wake wote watauawa humohumo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kweli siku zaja, nitakapoadhibu sanamu za Babuloni; nchi yake yote itatiwa aibu, watu wake wote watauawa humohumo. Neno: Bibilia Takatifu Kwa kuwa hakika wakati utawadia nitakapoziadhibu sanamu za Babeli; nchi yake yote itatiwa aibu, na watu wake wote waliouawa wataangukia ndani yake. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa kuwa hakika wakati utawadia nitakapoziadhibu sanamu za Babeli; nchi yake yote itatiwa aibu, na watu wake wote waliouawa wataangukia ndani yake. BIBLIA KISWAHILI Basi angalia, siku zitakuja, ambazo katika siku hizo, nitafanya hukumu juu ya sanamu za Babeli, na nchi yake yote itatahayarika; na watu wake wote waliouawa wataanguka katikati yake. |
Na, tazama, linakuja kundi la watu, wapanda farasi, wakienda wawili wawili. Akajibu na kusema, Babeli umeanguka, umeanguka; na sanamu zote za miungu yake zimevunjwa chini.
Kwa sababu hiyo BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, nitawaadhibu watu hawa; vijana watakufa kwa upanga; wana wao na binti zao watakufa kwa njaa;
Utasema nini wewe, atakapowaweka rafiki zako kuwa kichwa juu yako, ikiwa wewe mwenyewe umewafundisha kuwa juu yako? Je! Huzuni haitakushika, kama uchungu wa mwanamke aliye katika kuzaa?
Na katika habari ya nabii, na kuhani, na watu, watakaosema, Mzigo wa BWANA, mimi nitamwadhibu mtu yule, na nyumba yake.
Na itakuwa miaka hiyo sabini itakapotimia, nitamwadhibu mfalme wa Babeli, na taifa lile, asema BWANA, kwa sababu ya uovu wao, na nchi ya Wakaldayo pia; nami nitaifanya kuwa ukiwa wa milele.
Tangazeni katika mataifa, Mkahubiri na kutweka bendera; Hubirini, msifiche, semeni, Babeli umetwaliwa! Beli amefedheheka; Merodaki amefadhaika; Sanamu zake zimeaibishwa, Vinyago vyake vimefadhaika.
Nami nitamlipa Babeli, na wote wakaao ndani ya Ukaldayo, mabaya yao yote, waliyoyatenda katika Sayuni mbele ya macho yenu, asema BWANA.
Miji yake imekuwa maganjo; Nchi ya ukame, na jangwa; Nchi asimokaa mtu yeyote, Wala hapiti mwanadamu huko.
Kwa sababu hiyo siku zinakuja, asema BWANA, nitakapozihukumu sanamu zake; na katika nchi yake yote waliojeruhiwa wataomboleza.