Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Yeremia 51:43 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Miji yake imekuwa maganjo; Nchi ya ukame, na jangwa; Nchi asimokaa mtu yeyote, Wala hapiti mwanadamu huko.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Miji yake imekuwa kinyaa, nchi ya ukavu na jangwa, nchi isiyokaliwa na mtu yeyote, wala kupitika na binadamu yeyote.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Miji yake imekuwa kinyaa, nchi ya ukavu na jangwa, nchi isiyokaliwa na mtu yeyote, wala kupitika na binadamu yeyote.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Miji yake imekuwa kinyaa, nchi ya ukavu na jangwa, nchi isiyokaliwa na mtu yeyote, wala kupitika na binadamu yeyote.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Miji yake itakuwa ukiwa, kame na jangwa, nchi isiyokuwa na mtu anayeishi ndani yake, ambayo hakuna mwanadamu atakayepita humo.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Miji yake itakuwa ukiwa, kame na jangwa, nchi ambayo hakuna yeyote anayeishi ndani yake, ambayo hakuna mtu anayepita humo.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Miji yake imekuwa maganjo; Nchi ya ukame, na jangwa; Nchi asimokaa mtu yeyote, Wala hapiti mwanadamu huko.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Yeremia 51:43
12 Marejeleo ya Msalaba  

Njoni muyatazame matendo ya BWANA, Jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi.


Hautakaliwa na watu tena kabisa, wala watu hawatakaa ndani yake tangu kizazi hata kizazi. Mwarabu hatapiga hema yake huko, wala wachungaji hawatalaza makundi yao huko.


Miiba itamea majumbani mwake, upupu na mbigili ndani ya maboma yake; nayo itakuwa kao la mbweha, na ua la mbuni.


Kwa sababu hiyo uovu utakupata; wala hutaweza kuuagua; na msiba utakuangukia; hutaweza kuuondoa; na ukiwa usioujua utakupata kwa ghafla.


ili kufanya nchi yao kuwa kitu cha kushangaza, na cha kuzomewa daima; kila mtu apitaye karibu nayo atashangaa, na kutikisa kichwa chake.


Wala hawakusema, Yuko wapi BWANA, aliyetutoa katika nchi ya Misri; akatuongoza jangwani, katika nchi ya ukame na mashimo, katika nchi ya kiu na ya kivuli cha mauti, katika nchi ambayo ndani yake hapiti mtu, wala haikukaliwa na watu?


mama yenu atatahayarika sana; yeye aliyewazaa atafadhaika; tazama, atakuwa taifa lililo nyuma katika mataifa yote, atakuwa jangwa, nchi ya ukame, na nyika.


Nayo nchi yatetemeka, nayo ina uchungu; maana makusudi ya BWANA juu ya Babeli yasimama, kuifanya nchi ya Babeli ukiwa, isikaliwe na mtu.


Na Babeli utakuwa magofu, makao ya mbwamwitu, ajabu, na mazomeo, pasipo mtu wa kukaa huko.


ukaseme, Ee BWANA, umenena kuhusu mji huu kwamba utakatiliwa mbali, usikaliwe na awaye yote, wala wanadamu wala wanyama, lakini uwe ukiwa hata milele.