Yeremia 51:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nao wataanguka, wakiwa wameuawa, katika nchi ya Wakaldayo, wakiwa wametumbuliwa katika njia zake kuu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wataanguka na kuuawa katika nchi ya Wakaldayo, watajeruhiwa katika barabara zake. Biblia Habari Njema - BHND Wataanguka na kuuawa katika nchi ya Wakaldayo, watajeruhiwa katika barabara zake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wataanguka na kuuawa katika nchi ya Wakaldayo, watajeruhiwa katika barabara zake. Neno: Bibilia Takatifu Wataanguka barabarani waliouawa katika nchi ya Wakaldayo, wakiwa na majeraha ya kutisha. Neno: Maandiko Matakatifu Wataanguka waliouawa katika Babeli, wakiwa na majeraha ya kutisha barabarani zake. BIBLIA KISWAHILI Nao wataanguka, wakiwa wameuawa, katika nchi ya Wakaldayo, wakiwa wametumbuliwa katika njia zake kuu. |
Bali wewe umetupwa mbali na kaburi lako, Kama chipukizi lililochukiza kabisa; Kama vazi la wale waliouawa, Wale waliochomwa kwa upanga, Wale washukao mpaka misingi ya shimo; Kama mzoga uliokanyagwa chini ya miguu.
Kwa hiyo vijana wake wataanguka katika njia zake kuu, na watu wote wa vita watanyamazishwa katika siku hiyo, asema BWANA wa majeshi.
Kwa sababu hiyo vijana wake wataanguka katika njia zake kuu, na watu wake wa vita, wote pia, watanyamazishwa katika siku hiyo, asema BWANA.
Upanga uko juu ya farasi wao, na juu ya magari yao ya vita; na juu ya watu wote waliochanganyika ndani yake, nao watakuwa kama wanawake; upanga u juu ya hazina zake, nazo zitaibwa.
Babeli ujapopanda mbinguni, na ujapopafanya mahali pa juu penye nguvu zake kuwa ngome, hata hivyo toka kwangu wenye kuangamiza watamwendea, asema BWANA.