Ee BWANA, Mungu wangu, uangalie, uniitikie; Uyatie nuru macho yangu, Nisije nikalala usingizi wa mauti.
Yeremia 51:39 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wakiingiwa na ukali, nitawafanyia karamu yao, nami nitawalevya, wapate kufurahi, na kulala usingizi wa milele, wasiamke tena, asema BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakiwa na uchu mkubwa nitawaandalia karamu: Nitawalewesha mpaka wapepesuke; nao watalala usingizi wa daima na hawataamka tena. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Biblia Habari Njema - BHND Wakiwa na uchu mkubwa nitawaandalia karamu: Nitawalewesha mpaka wapepesuke; nao watalala usingizi wa daima na hawataamka tena. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakiwa na uchu mkubwa nitawaandalia karamu: nitawalewesha mpaka wapepesuke; nao watalala usingizi wa daima na hawataamka tena. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Neno: Bibilia Takatifu Lakini wakiwa wameamshwa, nitawaandalia karamu na kuwafanya walewe, ili washangilie kwa kicheko, kisha walale milele na wasiamke,” asema Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini wakati wakiwa wameamshwa, nitawaandalia karamu na kuwafanya walewe, ili wapige kelele kwa kicheko, kisha walale milele na wasiamke,” asema bwana. BIBLIA KISWAHILI Wakiingiwa na ukali, nitawafanyia karamu yao, nami nitawalevya, wapate kufurahi, na kulala usingizi wa milele, wasiamke tena, asema BWANA. |
Ee BWANA, Mungu wangu, uangalie, uniitikie; Uyatie nuru macho yangu, Nisije nikalala usingizi wa mauti.
Nawe utawaambia hivi, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nyweni, na kulewa, na kutapika, na kuanguka msiinuke tena, kwa sababu ya upanga nitakaoutuma kati yenu.
na Moabu atagaagaa katika matapiko yake, naye atadhihakiwa. Kwa maana Israeli, je! Hakuwa dhihaka kwako?
Nami nitawalevya wakuu wake, na watu wake wenye hekima, watawala wake, na makamanda wake, na mashujaa wake; nao watalala usingizi wa milele, wasiamke, asema Mfalme, BWANA wa majeshi, ambaye jina lake ni BWANA.
Wachungaji wako wanalala usingizi, Ee mfalme wa Ashuru; watu wako wenye heshima wamepumzika; watu wako wametawanyika juu ya milima, wala hapana mtu wa kuwakusanya.