Yeremia 51:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA ameitokeza haki yetu; Njooni, tutangaze katika Sayuni Habari za kazi ya BWANA, Mungu wetu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu amethibitisha kuwa hatuna hatia. Twendeni Siyoni tukatangaze matendo ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu amethibitisha kuwa hatuna hatia. Twendeni Siyoni tukatangaze matendo ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu amethibitisha kuwa hatuna hatia. Twendeni Siyoni tukatangaze matendo ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu. Neno: Bibilia Takatifu “ ‘Mwenyezi Mungu amethibitisha haki yetu; njooni, tutangaze katika Sayuni kitu ambacho Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, amefanya.’ Neno: Maandiko Matakatifu “ ‘bwana amethibitisha haki yetu; njooni, tutangaze katika Sayuni kitu ambacho bwana Mwenyezi Mungu wetu amefanya.’ BIBLIA KISWAHILI BWANA ameitokeza haki yetu; Njooni, tutangaze katika Sayuni Habari za kazi ya BWANA, Mungu wetu. |
Njoni, sikieni, ninyi nyote mnaomcha Mungu, Nami nitayatangaza aliyonitendea roho yangu.
Ili nizisimulie sifa zako zote; Katika malango ya binti Sayuni Nitaufurahia wokovu wako.
Hawa watainua sauti zao, watapiga kelele; kwa sababu ya utukufu wa BWANA watapiga kelele toka baharini.
Semeni na moyo wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa BWANA adhabu maradufu kwa dhambi zake zote.
Nao waliokombolewa na BWANA watarejea, Watafika Sayuni, wakiimba; Furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; Watapata shangwe na furaha; Huzuni na kuugua zitakimbia.
Sauti yao wakimbiao na kuokoka, Kutoka katika nchi ya Babeli, Ili kutangaza katika Sayuni kisasi cha BWANA, Mungu wetu, Kisasi cha hekalu lake.
Basi, lisikieni shauri la BWANA, Alilolifanya juu ya Babeli; Na makusudi yake aliyoyakusudia Juu ya nchi ya Wakaldayo. Hakika watawaburura, naam, wadogo wa kundi; Hakika malisho yao yatafadhaika kwa ajili yao.