Yeremia 50:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Watu wote waliowaona wamewala; na adui zao walisema, Sisi hatuna hatia, kwa kuwa hao wametenda dhambi juu ya BWANA, aliye kao la haki, yaani, BWANA, tumaini la baba zao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wote waliowakuta waliwaua, na maadui zao wamesema, ‘Hatuna hatia sisi’, maana hao wamemkosea Mwenyezi-Mungu aliye malisho yao ya kweli; Mwenyezi-Mungu ambaye ni tegemeo la wazee wao! Biblia Habari Njema - BHND Watu wote waliowakuta waliwaua, na maadui zao wamesema, ‘Hatuna hatia sisi’, maana hao wamemkosea Mwenyezi-Mungu aliye malisho yao ya kweli; Mwenyezi-Mungu ambaye ni tegemeo la wazee wao! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wote waliowakuta waliwaua, na maadui zao wamesema, ‘Hatuna hatia sisi’, maana hao wamemkosea Mwenyezi-Mungu aliye malisho yao ya kweli; Mwenyezi-Mungu ambaye ni tegemeo la wazee wao! Neno: Bibilia Takatifu Yeyote aliyewakuta aliwala; adui zao walisema, ‘Sisi hatuna hatia, kwa kuwa wao walitenda dhambi dhidi ya Mwenyezi Mungu, malisho yao halisi, Mwenyezi Mungu, aliye tumaini la baba zao.’ Neno: Maandiko Matakatifu Yeyote aliyewakuta aliwala; adui zao walisema, ‘Sisi hatuna hatia, kwa kuwa wao walitenda dhambi dhidi ya bwana, malisho yao halisi, bwana, aliye tumaini la baba zao.’ BIBLIA KISWAHILI Watu wote waliowaona wamewala; na adui zao walisema, Sisi hatuna hatia, kwa kuwa hao wametenda dhambi juu ya BWANA, aliye kao la haki, yaani, BWANA, tumaini la baba zao. |
Nilikuwa nimekasirika na watu wangu, niliutia unajisi urithi wangu, nikawatia mkononi mwako; wewe hukuwatendea rehema; kwa wazee uliifanya nira yako kuwa nzito sana.
Waashuri upande wa mbele, na Wafilisti upande wa nyuma, nao watamla Israeli kwa kinywa kilicho wazi. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.
Hasira yako uwamwagie mataifa wasiokujua, na jamaa zao wasioliitia jina lako; kwa maana wamemla Yakobo, naam, wamemla kabisa na kumwangamiza, na kuyafanya makao yake kuwa ukiwa.
Wewe uliye tumaini la Israeli, wewe uliye Mwokozi wake wakati wa taabu, kwa nini wewe umekuwa kama mtu akaaye katika nchi, kama mgeni, na kama mtu mwenye kusafiri, ageukaye upande ili kukaa usiku mmoja tu?
Ee BWANA, tumaini la Israeli, wote wakuachao watatahayarika. Wao watakaojitenga nami wataandikwa katika mchanga, kwa sababu wamemwacha BWANA, kisima cha maji yaliyo hai.
Israeli walikuwa utakatifu kwa BWANA; malimbuko ya uzao wake; Wote watakaomla watakuwa na hatia; uovu utawajia; asema BWANA.
BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Watatumia tena neno hili katika nchi ya Yuda, na katika miji yake, nitakapowarudisha mateka yao; BWANA na akubariki, Ee makao ya haki, Ee mlima wa utakatifu.
Katika siku zile, na wakati ule, nitamchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atafanya hukumu na haki katika nchi hii.
Katika siku zile Yuda ataokolewa, na Yerusalemu utakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, BWANA ni haki yetu.
Nao watakula mavuno yako, na mkate wako, ambao iliwapasa wana wako na binti zako kuula; watakula makundi yako ya kondoo na ya ng'ombe; watakula mizabibu yako na mitini yako; wataiharibu miji yako yenye boma, uliyokuwa ukiitumainia, naam, wataiharibu kwa upanga.
Jipangeni juu ya Babeli pande zote, Ninyi nyote mpindao upinde; Mpigeni, msiuzuie hata mshale mmoja; Kwa maana amemtenda BWANA dhambi.
Israeli ni kondoo aliyetawanywa; simba wamemfukuzia mbali; kwanza mfalme wa Ashuru amemla, na mwisho Nebukadneza huyu, mfalme wa Babeli, amemvunja mifupa yake.
BWANA wa majeshi asema hivi, Wana wa Israeli, na wana wa Yuda wameonewa sana, na pia wana wa Yuda vivyo hivyo, watekaji wao wote wamewashikilia sana; na wamekataa kuwaachilia waondoke.
Nao wakatawanyika, kwa sababu hapakuwa na mchungaji; wakawa chakula cha wanyamamwitu, wakatawanyika.
Nawe utajua ya kuwa mimi, BWANA, nimeyasikia matusi yako yote, uliyoyanena juu ya milima ya Israeli, ukisema, Wamefanyika ukiwa, wametiwa katika mikono yetu tuwale.
Ee Bwana sawasawa na haki yako yote, nakusihi, hasira yako na ghadhabu yako zigeuzwe na kuuacha mji wako Yerusalemu, mlima wako mtakatifu; maana kwa sababu ya dhambi zetu, na maovu ya baba zetu, Yerusalemu na watu wako wamepata kulaumiwa na watu wote wanaotuzunguka.
wala hatukuwasikiliza watumishi wako, manabii, ambao kwa jina lako walisema na wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, na watu wote wa nchi.
Nami ninayakasirikia sana mataifa yanayostarehe; kwa maana mimi nilikuwa nimekasirika kidogo tu, nao wakayazidisha maafa.
ambalo wenye kundi hilo huwachinja, kisha hujiona kuwa hawana hatia; na hao wawauzao husema, Na ahimidiwe BWANA, kwa maana mimi ni tajiri; na wachungaji wao wenyewe hawawahurumii.
Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na Kristo Yesu, tarajio letu;