Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Yeremia 50:39 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Basi, wanyama wakali wa jangwani, pamoja na mbwamwitu, watakaa huko, na mbuni watakaa ndani yake; wala haitakaliwa na watu milele; wala hakuna mtu atakayekaa huko tangu kizazi hadi kizazi.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

“Kwa hiyo wanyama wa porini, mbwamwitu pamoja na mbuni, watakaa Babuloni. Hapatakaliwa kamwe na watu vizazi vyote vijavyo.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

“Kwa hiyo wanyama wa porini, mbwamwitu pamoja na mbuni, watakaa Babuloni. Hapatakaliwa kamwe na watu vizazi vyote vijavyo.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

“Kwa hiyo wanyama wa porini, mbwamwitu pamoja na mbuni, watakaa Babuloni. Hapatakaliwa kamwe na watu vizazi vyote vijavyo.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

“Kwa hiyo, viumbe vya jangwani na fisi wataishi humo, nao bundi watakaa humo. Kamwe haitakaliwa tena wala watu hawataishi humo kizazi hadi kizazi.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

“Kwa hiyo, viumbe vya jangwani na fisi wataishi humo, nao bundi watakaa humo. Kamwe haitakaliwa tena wala watu hawataishi humo kutoka kizazi hadi kizazi.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Basi, wanyama wakali wa jangwani, pamoja na mbwamwitu, watakaa huko, na mbuni watakaa ndani yake; wala haitakaliwa na watu milele; wala hakuna mtu atakayekaa huko tangu kizazi hadi kizazi.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Yeremia 50:39
12 Marejeleo ya Msalaba  

Tena nitaifanya hiyo nchi kuwa makao ya nungunungu, na maziwa ya maji; nami nitaifagilia mbali kwa ufagio wa uharibifu; asema BWANA wa majeshi.

Na itakuwa miaka hiyo sabini itakapotimia, nitamwadhibu mfalme wa Babeli, na taifa lile, asema BWANA, kwa sababu ya uovu wao, na nchi ya Wakaldayo pia; nami nitaifanya kuwa ukiwa wa milele.

Maana toka kaskazini taifa linakuja juu yake, litakaloifanya nchi yake kuwa ukiwa; wala hakuna mtu atakayekaa humo; wamekimbia, wamekwenda zao, mwanadamu na mnyama pia.

Wala hawatatwaa kwako jiwe moja liwe la pembeni, wala jiwe moja liwe msingi; bali wewe utakuwa ukiwa daima, asema BWANA.

Miji yake imekuwa maganjo; Nchi ya ukame, na jangwa; Nchi asimokaa mtu yeyote, Wala hapiti mwanadamu huko.

Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ulio mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;