Na Mungu akamkumbuka Nuhu, na kila kilicho hai, na wanyama wote waliokuwamo pamoja naye katika safina; Mungu akavumisha upepo juu ya nchi, maji yakapungua;
Yeremia 50:38 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ukosefu wa mvua uko juu ya maji yake, nayo yatakaushwa; maana ni nchi ya sanamu za kuchongwa, nao wameingiwa na wazimu kwa ajili ya sanamu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ukame uyapate maji ili yapate kukauka! Maana Babuloni ni nchi ya sanamu za miungu, watu ni wendawazimu juu ya vinyago vyao. Biblia Habari Njema - BHND Ukame uyapate maji ili yapate kukauka! Maana Babuloni ni nchi ya sanamu za miungu, watu ni wendawazimu juu ya vinyago vyao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ukame uyapate maji ili yapate kukauka! Maana Babuloni ni nchi ya sanamu za miungu, watu ni wendawazimu juu ya vinyago vyao. Neno: Bibilia Takatifu Ukame juu ya maji yake! Nayo yatakauka. Kwa kuwa ni nchi ya sanamu, wao wanaenda wazimu kwa ajili ya sanamu. Neno: Maandiko Matakatifu Ukame juu ya maji yake! Nayo yatakauka. Kwa kuwa ni nchi ya sanamu, wao wanaenda wazimu kwa ajili ya sanamu. BIBLIA KISWAHILI Ukosefu wa mvua uko juu ya maji yake, nayo yatakaushwa; maana ni nchi ya sanamu za kuchongwa, nao wameingiwa na wazimu kwa ajili ya sanamu. |
Na Mungu akamkumbuka Nuhu, na kila kilicho hai, na wanyama wote waliokuwamo pamoja naye katika safina; Mungu akavumisha upepo juu ya nchi, maji yakapungua;
Nizitanguaye ishara za waongo, na kuwatia waganga wazimu; niwarudishaye nyuma wenye hekima, na kuyageuza maarifa yao kuwa ujinga;
mama yenu atatahayarika sana; yeye aliyewazaa atafadhaika; tazama, atakuwa taifa lililo nyuma katika mataifa yote, atakuwa jangwa, nchi ya ukame, na nyika.
Tangazeni katika mataifa, Mkahubiri na kutweka bendera; Hubirini, msifiche, semeni, Babeli umetwaliwa! Beli amefedheheka; Merodaki amefadhaika; Sanamu zake zimeaibishwa, Vinyago vyake vimefadhaika.
Nami nitafanya hukumu juu ya Beli katika Babeli, nami nitavitoa katika kinywa chake alivyovimeza; wala mataifa hawatamwendea tena; naam, ukuta wa Babeli utaanguka.
Basi angalia, siku zitakuja, ambazo katika siku hizo, nitafanya hukumu juu ya sanamu za Babeli, na nchi yake yote itatahayarika; na watu wake wote waliouawa wataanguka katikati yake.
Kwa sababu hiyo siku zinakuja, asema BWANA, nitakapozihukumu sanamu zake; na katika nchi yake yote waliojeruhiwa wataomboleza.
Babeli umekuwa kikombe cha dhahabu mkononi mwa BWANA; kilicholevya dunia yote; mataifa wamekunywa mvinyo wake; kwa sababu hiyo mataifa wameingiwa na wazimu.
Wakanywa divai, wakaisifu miungu ya dhahabu, na ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe.
Paulo alipokuwa akiwangojea huko Athene na kuona jinsi mji ule ulivyojaa sanamu, roho yake ilichukizwa sana ndani yake.
Na huyo wa sita akalimimina bakuli lake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.
Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, Babeli MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.
Ndipo wakazi wa mji wakamwambia Yoashi, Mlete mwanao, afe; kwa sababu ameibomoa madhabahu ya Baali na kwa sababu ameikata ile Ashera iliyokuwa karibu nayo.