Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Yeremia 50:31 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Tazama, mimi ni juu yako, Ewe mwenye kiburi, asema Bwana, BWANA wa majeshi; maana siku yako imewadia, wakati nitakapokujia.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

“Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, napigana nawe ewe mwenye kiburi, maana siku yako ya adhabu imefika, wakati nitakapokuadhibu umewadia.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

“Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, napigana nawe ewe mwenye kiburi, maana siku yako ya adhabu imefika, wakati nitakapokuadhibu umewadia.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

“Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, napigana nawe ewe mwenye kiburi, maana siku yako ya adhabu imefika, wakati nitakapokuadhibu umewadia.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

“Tazama, niko kinyume nawe, ewe mwenye majivuno,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, “kwa kuwa siku yako imewadia, yaani wakati wako wa kuadhibiwa.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

“Tazama, niko kinyume nawe, ewe mwenye majivuno,” asema Bwana, bwana Mwenye Nguvu Zote, “kwa kuwa siku yako imewadia, yaani, wakati wako wa kuadhibiwa.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Tazama, mimi ni juu yako, Ewe mwenye kiburi, asema Bwana, BWANA wa majeshi; maana siku yako imewadia, wakati nitakapokujia.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Yeremia 50:31
20 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana kutakuwa siku ya BWANA wa majeshi juu ya watu wote wenye kiburi na majivuno, na juu ya yote yaliyoinuka; nayo yatashushwa chini.


Tazama, mimi niko juu yako, Ewe ukaaye bondeni, na kwenye jabali la uwandani, asema BWANA ninyi mnaosema, Ni nani atakayeshuka apigane nasi? Au, Ni nani atakayeingia katika makao yetu?


Tumesikia habari za kiburi cha Moabu; Ya kuwa ana kiburi kingi; Ujeuri wake, na kiburi chake, na majivuno yake, Na jinsi alivyojitukuza moyoni mwake.


Kuhusu kuogofya kwako, Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Ushikaye kilele cha milima; Ujapofanya kiota chako juu sana kama tai, Nitakushusha kutoka huko; asema BWANA.


Waiteni wapiga mishale juu ya Babeli, Naam, wote waupindao upinde; Pangeni hema kumzunguka pande zote; Ili asiokoke hata mtu mmoja wao; Mlipeni kwa kadiri ya kazi yake; Mtendeni sawasawa na yote aliyoyatenda; Kwa sababu amefanya kiburi juu ya BWANA, Juu yake aliye Mtakatifu wa Israeli.


Na mwenye kiburi atajikwaa, na kuanguka, wala hapana atakayemwinua; nami nitawasha moto katika miji yake, nao utawala wote wamzungukao pande zote.


Tazama, mimi niko juu yako, Ee mlima uharibuo, asema BWANA; wewe uiharibuye dunia nzima; nami nitaunyosha mkono wangu juu yako, na kukubingirisha chini toka majabalini; nami nitakufanya kuwa mlima ulioteketezwa.


nena, useme, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ewe Farao, mfalme wa Misri, joka kubwa aoteaye kati ya mito yake, aliyesema, Mto wangu ni wangu mwenyewe, nami nimeufanya kwa ajili ya nafsi yangu.


useme, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ewe Gogu, mkuu wa Roshi, na Mesheki, na Tubali;


Na wewe, mwanadamu, tabiri juu ya Gogu, useme, Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, mimi ni juu yako, Ewe Gogu, mkuu wa Roshi, Mesheki, na Tubali;


basi, Bwana MUNGU asema hivi; Angalia, mimi, naam, mimi, ni juu yako; nami nitafanya hukumu kati yako machoni pa mataifa.


Tazama, mimi ni juu yako, asema BWANA wa majeshi, nami nitayateketeza magari yako ya vita katika moshi, na upanga utawaangamiza wanasimba wako; nami nitayakatilia mbali mawindo yako katika nchi, na sauti za wajumbe wako hazitasikiwa tena kamwe.


Tazama, mimi ni juu yako, asema BWANA wa majeshi; nami nitayainua marinda yako mbele ya uso wako; nami nitawaonesha mataifa uchi wako, na falme aibu yako.


Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.


Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.


Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu.