BWANA akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewaumba.
Yeremia 50:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana toka kaskazini taifa linakuja juu yake, litakaloifanya nchi yake kuwa ukiwa; wala hakuna mtu atakayekaa humo; wamekimbia, wamekwenda zao, mwanadamu na mnyama pia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Kwa maana, taifa kutoka kaskazini limefika kuushambulia; litaifanya nchi yake kuwa uharibifu. Hakuna atakeyeishi humo; watu na wanyama watakimbia mbali. Biblia Habari Njema - BHND “Kwa maana, taifa kutoka kaskazini limefika kuushambulia; litaifanya nchi yake kuwa uharibifu. Hakuna atakeyeishi humo; watu na wanyama watakimbia mbali. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Kwa maana, taifa kutoka kaskazini limefika kuushambulia; litaifanya nchi yake kuwa uharibifu. Hakuna atakeyeishi humo; watu na wanyama watakimbia mbali. Neno: Bibilia Takatifu Taifa kutoka kaskazini litamshambulia, na kuifanya nchi yake ukiwa. Hakuna atakayeishi ndani yake, watu na wanyama wataikimbia. Neno: Maandiko Matakatifu Taifa kutoka kaskazini litamshambulia, na kuifanya nchi yake ukiwa. Hakuna hata mmoja atakayeishi ndani yake, watu na wanyama wataikimbia. BIBLIA KISWAHILI Maana toka kaskazini taifa linakuja juu yake, litakaloifanya nchi yake kuwa ukiwa; wala hakuna mtu atakayekaa humo; wamekimbia, wamekwenda zao, mwanadamu na mnyama pia. |
BWANA akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewaumba.
Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawaua wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA.
Nimemwinua mtu toka kaskazini, naye amekuja; toka maawio ya jua amekuja anitajaye jina langu; naye atawakanyaga watawala kama akanyagaye matope, na kama mfinyanzi apondaye udongo.
Haya ndiyo BWANA amwambiayo Koreshi, masihi wake, ambaye nimemshika mkono wake wa kulia, ili kutiisha mataifa mbele yake, nami nitalegeza nguvu za wafalme; ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa.
Kwa maana juu ya Babeli nitaamsha na kuleta kusanyiko la mataifa makubwa, toka nchi ya kaskazini; nao watajipanga juu yake; kutoka huko atatwaliwa; mishale yao itakuwa kama ya mtu shujaa aliye stadi; hakuna hata mmoja utakaorudi bure.
Inoeni hiyo mishale; zishikeni ngao kwa nguvu; BWANA ameziamsha roho za wafalme wa Wamedi; kwa sababu shauri lake ni juu ya Babeli auangamize; maana ni kisasi cha BWANA, kisasi cha hekalu lake.
Ndipo mbingu, na nchi, na vitu vyote vilivyomo, vitaimba kwa furaha juu ya Babeli; kwa maana watu waangamizao watamjia kutoka kaskazini, asema BWANA.
ukaseme, Ee BWANA, umenena kuhusu mji huu kwamba utakatiliwa mbali, usikaliwe na awaye yote, wala wanadamu wala wanyama, lakini uwe ukiwa hata milele.
Kwa hiyo, Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, hasira yangu na ghadhabu yangu zitamwagwa juu ya mahali hapa, juu ya wanadamu, na juu ya wanyama, na juu ya miti ya mashamba, na juu ya mazao ya nchi; nayo itateketea, isizimike.
Kwa milima nitalia na kulalama, Na kwa malisho ya nyikani nitafanya maombolezo; Kwa sababu yameteketea, hata hakuna apitaye, Wala hapana awezaye kusikia sauti ya ng'ombe; Ndege wa angani, na wanyama wa mwituni, Wamekimbia, wamekwenda zao.
Nami nitafanya Yerusalemu kuwa magofu, Makao ya mbweha; Nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, Isikaliwe na mtu awaye yote.
Nitamkomesha mwanadamu na mnyama; nitakomesha ndege wa angani, na samaki wa baharini, na hayo yakwazayo pamoja na waovu; nami nitamkatilia mbali mwanadamu, asionekane juu ya uso wa nchi, asema BWANA.