Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Yeremia 50:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Sauti yao wakimbiao na kuokoka, Kutoka katika nchi ya Babeli, Ili kutangaza katika Sayuni kisasi cha BWANA, Mungu wetu, Kisasi cha hekalu lake.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

“Sikiliza! Wakimbizi na watoro kutoka nchi ya Babuloni wanakuja kutangaza huko Siyoni jinsi Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, alivyolipiza kisasi kwa ajili ya hekalu lake.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

“Sikiliza! Wakimbizi na watoro kutoka nchi ya Babuloni wanakuja kutangaza huko Siyoni jinsi Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, alivyolipiza kisasi kwa ajili ya hekalu lake.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

“Sikiliza! Wakimbizi na watoro kutoka nchi ya Babuloni wanakuja kutangaza huko Siyoni jinsi Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, alivyolipiza kisasi kwa ajili ya hekalu lake.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Wasikilizeni watoro na wakimbizi kutoka Babeli wakitangaza katika Sayuni jinsi Mwenyezi Mungu, Mungu wetu alivyolipiza kisasi, kisasi kwa ajili ya Hekalu lake.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Wasikilizeni watoro na wakimbizi kutoka Babeli wakitangaza katika Sayuni jinsi bwana, Mungu wetu alivyolipiza kisasi, kisasi kwa ajili ya Hekalu lake.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Sauti yao wakimbiao na kuokoka, Kutoka katika nchi ya Babeli, Ili kutangaza katika Sayuni kisasi cha BWANA, Mungu wetu, Kisasi cha hekalu lake.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Yeremia 50:28
14 Marejeleo ya Msalaba  

Haya, tokeni katika Babeli, Kimbieni kutoka kwa Wakaldayo; Hubirini kwa sauti ya kuimba, tangazeni haya, Yatamkeni mpaka mwisho wa dunia, semeni, BWANA amemkomboa mtumishi wake, Yakobo.

Mpigieni kelele pande zote; amejitoa; Maboma yake yameanguka, kuta zake zimebomolewa; Kwa maana ni kisasi cha BWANA; mlipizeni kisasi; Kama yeye alivyotenda, mtendeni yeye.

Enyi watu wangu; tokeni katikati yake, mkajiokoe nafsi zenu kutoka kwa hasira kali ya BWANA, kila mmoja wenu.

Kimbieni kutoka kati ya Babeli, kila mtu na ajiokoe nafsi yake; msikatiliwe mbali katika uovu wake; maana ni wakati wa kisasi cha BWANA, atamlipa malipo.

Huyo mtesi amenyosha mkono wake Juu ya matamanio yake yote; Maana ameona ya kuwa mataifa wameingia Ndani ya patakatifu pake; Ambao kwa habari zao wewe uliamuru Wasiingie katika kusanyiko lako.

Bali umejiinua juu ya Bwana wa mbingu; nao wamevileta vyombo vya nyumba yake mbele yako; na wewe, na wakuu wako, na wake zako, na masuria wako, mmevinywea; nawe umeisifu miungu ya fedha na ya dhahabu na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe; wasioona, wala kusikia, wala kujua neno lolote; na Mungu yule, ambaye pumzi yako i mkononi mwake, na njia zako zote ni zake, hukumtukuza.

Nami nitaleta upanga juu yenu, utakaopatiliza kisasi cha hilo agano; nanyi mtakutanishwa ndani ya miji yenu; nami nitaleta tauni kati yenu; nanyi mtatiwa mikononi mwa adui.

Nikiunoa upanga wangu wa umeme, Mkono wangu ukishika hukumu, Nitawatoza kisasi adui zangu, Nitawalipa wanaonichukia.