Hao wanaokaa magharibi watastaajabia siku yake, Kama vile wanaokaa mashariki walivyotiwa hofu.
Yeremia 50:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wachinjeni mafahali wake wote; Na wateremkie machinjoni; Ole wao! Maana siku yao imewadia, Wakati wa kujiliwa kwao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waueni askari wake hodari; waache washukie machinjoni. Ole wao, maana siku yao imewadia, wakati wao wa kuadhibiwa umefika. Biblia Habari Njema - BHND Waueni askari wake hodari; waache washukie machinjoni. Ole wao, maana siku yao imewadia, wakati wao wa kuadhibiwa umefika. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waueni askari wake hodari; waache washukie machinjoni. Ole wao, maana siku yao imewadia, wakati wao wa kuadhibiwa umefika. Neno: Bibilia Takatifu Waueni mafahali wake wachanga wote; waacheni washuke machinjoni! Ole wao! Kwa kuwa siku yao imewadia, wakati wao wa kuadhibiwa. Neno: Maandiko Matakatifu Waueni mafahali wake wachanga wote; waacheni washuke machinjoni! Ole wao! Kwa kuwa siku yao imewadia, wakati wao wa kuadhibiwa. BIBLIA KISWAHILI Wachinjeni mafahali wake wote; Na wateremkie machinjoni; Ole wao! Maana siku yao imewadia, Wakati wa kujiliwa kwao. |
Hao wanaokaa magharibi watastaajabia siku yake, Kama vile wanaokaa mashariki walivyotiwa hofu.
Upanga wa BWANA umeshiba damu, umejazwa mafuta, kwa damu ya wana-kondoo na mbuzi, kwa mafuta ya figo za kondoo dume; maana BWANA ana dhabihu huko Bozra, machinjo makubwa katika nchi ya Edomu.
Na nyati watateremka pamoja nao, na ndama pamoja na mafahali, na nchi yao italewa kwa damu, na mavumbi yake yatanoneshwa kwa shahamu.
Lakini wewe, BWANA, wanijua; umeniona, umeujaribu moyo wangu, jinsi unavyokuelekea; uwakokote kama kondoo waendao kuchinjwa, ukawaweke tayari kwa siku ya kuchinjwa.
Ombolezeni, enyi wachungaji, na kulia; na kugaagaa katika majivu, enyi mlio hodari katika kundi; maana siku za kuuawa kwenu zimetimia kabisa, nami nitawavunja vipande vipande, nanyi mtaanguka kama chombo cha anasa.
Na mataifa yote watamtumikia yeye, na mwanawe, na mwana wa mwanawe, hata utakapowadia wakati wa nchi yake mwenyewe, ndipo mataifa mengi na wafalme wakuu watamtumikisha yeye.
Na askari wake waliojiwa, walio kati yake, Ni kama ndama walionona malishoni; Maana wao nao wamerudi nyuma, Wamekimbia wote pamoja, wasisimame; Maana siku ya msiba wao imewafikia, Wakati wa kujiliwa kwao.
Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya BWANA kwa ulegevu; na alaaniwe auzuiaye upanga wake usimwage damu.
Moabu ameharibika, na moshi wa miji yake umepanda; na vijana wake wateule wameteremka kwenda kuchinjwa, asema Mfalme, ambaye jina lake ni BWANA wa majeshi.
Aikimbiaye hofu ataanguka shimoni; na yeye atokaye shimoni atanaswa kwa mtego; maana nitaleta juu yake, yaani, juu ya Moabu, mwaka wa kujiliwa kwake, asema BWANA.
Kwa sababu mnafurahi, kwa sababu mnashangilia, enyi mnaouteka urithi wangu, kwa sababu mmenona kama mtamba akanyagaye nafaka, nanyi mnalia kama farasi wenye nguvu;
Tazama, mimi ni juu yako, Ewe mwenye kiburi, asema Bwana, BWANA wa majeshi; maana siku yako imewadia, wakati nitakapokujia.
Wamesikia kwamba napiga kite; Hakuna hata mmoja wa kunifariji; Adui zangu wote wamesikia habari ya mashaka yaliyonipata; Hufurahi kwa kuwa umeyafanya hayo; Utaileta siku ile uliyoitangaza, Nao watakuwa kama mimi.
wakisimama mbali kwa hofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio na nguvu! Kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja.
Kisha nikaona malaika mmoja amesimama katika jua; akalia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao katikati ya mbingu, Njooni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu;