Nitamtuma juu ya taifa lenye kukufuru, nitampa maagizo juu ya watu wa ghadhabu yangu, ateke nyara, na kuchukua mateka, na kuwakanyaga kama matope ya njiani.
Yeremia 50:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Njooni juu yake toka mpaka ulio mbali; Zifungueni ghala zake; Mfanyeni kuwa magofu na kumharibu kabisa; Msimsazie kitu chochote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Njoni mkamshambulie kutoka kila upande; zifungueni ghala zake za chakula; mrundikieni marundo ya nafaka! Iangamizeni kabisa nchi hii; msibakize chochote! Biblia Habari Njema - BHND Njoni mkamshambulie kutoka kila upande; zifungueni ghala zake za chakula; mrundikieni marundo ya nafaka! Iangamizeni kabisa nchi hii; msibakize chochote! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Njoni mkamshambulie kutoka kila upande; zifungueni ghala zake za chakula; mrundikieni marundo ya nafaka! Iangamizeni kabisa nchi hii; msibakize chochote! Neno: Bibilia Takatifu Njooni dhidi yake kutoka mbali. Zifungueni ghala zake za nafaka; mlundikeni kama lundo la nafaka. Mwangamizeni kabisa na msimwachie mabaki yoyote. Neno: Maandiko Matakatifu Njooni dhidi yake kutoka mbali. Zifungueni ghala zake za nafaka; mlundikeni kama lundo la nafaka. Mwangamizeni kabisa na msimwachie mabaki yoyote. BIBLIA KISWAHILI Njooni juu yake toka mpaka ulio mbali; Zifungueni ghala zake; Mfanyeni kuwa magofu na kumharibu kabisa; Msimsazie kitu chochote. |
Nitamtuma juu ya taifa lenye kukufuru, nitampa maagizo juu ya watu wa ghadhabu yangu, ateke nyara, na kuchukua mateka, na kuwakanyaga kama matope ya njiani.
Tena nitaifanya hiyo nchi kuwa makao ya nungunungu, na maziwa ya maji; nami nitaifagilia mbali kwa ufagio wa uharibifu; asema BWANA wa majeshi.
Kwa maana mkono wa BWANA utatulia katika mlima huu, na Moabu atakanyagwa chini huko aliko, kama vile majani makavu yakanyagwavyo katika maji machafu.
nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli.
Naye atawatolea ishara mataifa toka mbali, Naye atawapigia miruzi tokea mwisho wa nchi; Na tazama, watakuja mbio mbio upesi sana.
Kwa sababu ya ghadhabu ya BWANA haitakaliwa na mtu, bali itakuwa ukiwa mtupu; kila mtu apitaye karibu na Babeli atashangaa, atazomea kwa sababu ya mapigo yake yote.
Mpigieni kelele pande zote; amejitoa; Maboma yake yameanguka, kuta zake zimebomolewa; Kwa maana ni kisasi cha BWANA; mlipizeni kisasi; Kama yeye alivyotenda, mtendeni yeye.
Imekuwaje nyundo ya dunia yote Kukatiliwa mbali na kuvunjwa? Imekuwaje Babeli kuwa ukiwa Katikati ya mataifa?
Angalia, watu wanakuja watokao kaskazini; na taifa kubwa, na wafalme wengi wataamshwa toka pande za mwisho za dunia.
Nami nitafanya hukumu juu ya Beli katika Babeli, nami nitavitoa katika kinywa chake alivyovimeza; wala mataifa hawatamwendea tena; naam, ukuta wa Babeli utaanguka.
nawe utasema, Hivyo ndivyo utakavyozama Babeli, wala hautazuka tena, kwa sababu ya mabaya yote nitakayoleta juu yake; nao watachoka. Maneno ya Yeremia yamefika hata hapa.
Ndipo adui yangu ataliona jambo hilo, na aibu itamfunika, yeye aliyeniambia, Yuko wapi BWANA, Mungu wako? Macho yangu yatamtazama; sasa atakanyagwa kama matope ya njia kuu.
Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kuliko hao?
Malaika yule akautupa mundu wake hata nchi, akauchuma mzabibu wa nchi, akazitupa zabibu katika shinikizo hilo kubwa la ghadhabu ya Mungu.
Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili kwa upanga huo awapige mataifa. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.