Basi, itakuwa kama vile paa aliyetishwa, na kama kondoo wasio na mtu wa kuwakusanya; kila mtu atageukia watu wake; nao watakimbia, kila mtu aende nchi yake mwenyewe.
Yeremia 50:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mpanzi mkatilie mbali na Babeli, Naye ashikaye mundu wakati wa mavuno; Kwa sababu ya kuuogopa upanga uoneao, Watageuka kila mtu kwa watu wake, Nao wataikimbilia kila mmoja nchi yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Zuieni watu wasipande mbegu Babuloni, wala wasivune wakati wa mavuno. Kutokana na upanga wa udhalimu, kila mmoja atawarudia watu wake kila mmoja atakimbilia nchini mwake. Biblia Habari Njema - BHND Zuieni watu wasipande mbegu Babuloni, wala wasivune wakati wa mavuno. Kutokana na upanga wa udhalimu, kila mmoja atawarudia watu wake kila mmoja atakimbilia nchini mwake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Zuieni watu wasipande mbegu Babuloni, wala wasivune wakati wa mavuno. Kutokana na upanga wa udhalimu, kila mmoja atawarudia watu wake kila mmoja atakimbilia nchini mwake. Neno: Bibilia Takatifu Katilieni mbali mpanzi kutoka Babeli, pamoja na mvunaji na mundu wake akivuna. Kwa sababu ya upanga wa mdhalimu kila mmoja na arejee kwa watu wake mwenyewe, kila mmoja na akimbilie kwenye nchi yake mwenyewe. Neno: Maandiko Matakatifu Katilieni mbali mpanzi kutoka Babeli, pamoja na mvunaji na mundu wake akivuna. Kwa sababu ya upanga wa mdhalimu kila mmoja na arejee kwa watu wake mwenyewe, kila mmoja na akimbilie kwenye nchi yake mwenyewe. BIBLIA KISWAHILI Mpanzi mkatilie mbali na Babeli, Naye ashikaye mundu wakati wa mavuno; Kwa sababu ya kuuogopa upanga uoneao, Watageuka kila mtu kwa watu wake, Nao wataikimbilia kila mmoja nchi yake. |
Basi, itakuwa kama vile paa aliyetishwa, na kama kondoo wasio na mtu wa kuwakusanya; kila mtu atageukia watu wake; nao watakimbia, kila mtu aende nchi yake mwenyewe.
Ameacha mahali pake pa kujificha, kama simba; maana nchi yao imekuwa kitu cha kushangaza, kwa sababu ya ukali wa upanga uoneao, na kwa sababu ya hasira yake kali.
Aliwakwaza wengi, naam, wakaangukiana wao kwa wao; wakasema, Haya! Na tuondoke, tukarudi kwa watu wetu wenyewe, hadi nchi tuliyozaliwa, tuukimbie upanga unaotuonea.
na kwa wewe nitamvunjavunja mchungaji na kundi lake; na kwa wewe nitamvunjavunja mkulima na jozi yake ya ng'ombe; na kwa wewe nitawavunjavunja watawala na makamanda.
Tungependa kuuponya Babeli, Lakini haukuponyeka; Mwacheni, nasi twendeni zetu, Kila mtu hata nchi yake mwenyewe; Maana hukumu yake inafika hata mbinguni, Nayo imeinuliwa kufikia mawinguni.
Tahayarini, enyi wakulima; Pigeni yowe, enyi watunzaji wa mizabibu; Kwa ajili ya ngano na shayiri, Maana mavuno ya mashamba yamepotea.
Kwa ajili ya hayo, asema BWANA, Mungu wa majeshi, aliye Bwana; Kutakuwako maombolezo katika njia kuu zote; nao watasema katika njia zote, Ole! Ole! Nao watamwita mkulima aje kuombolea, na hao walio hodari wa kulia waje kuomboleza.