Tena nitaifanya hiyo nchi kuwa makao ya nungunungu, na maziwa ya maji; nami nitaifagilia mbali kwa ufagio wa uharibifu; asema BWANA wa majeshi.
Yeremia 49:33 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na Hazori utakuwa kao la mbwamwitu; ukiwa milele; hakuna mtu atakayekaa huko, wala hakuna mwanadamu atakayekaa huko kama mgeni akaavyo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mji wa Hazori utakuwa makao ya mbweha, utakuwa jangwa daima; hakuna mtu atakayekaa humo, wala atakayeishi humo.” Biblia Habari Njema - BHND Mji wa Hazori utakuwa makao ya mbweha, utakuwa jangwa daima; hakuna mtu atakayekaa humo, wala atakayeishi humo.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mji wa Hazori utakuwa makao ya mbweha, utakuwa jangwa daima; hakuna mtu atakayekaa humo, wala atakayeishi humo.” Neno: Bibilia Takatifu “Hazori itakuwa makao ya mbweha, mahali pa ukiwa milele. Hakuna atakayeishi humo; hakuna mtu atakayekaa ndani yake.” Neno: Maandiko Matakatifu “Hazori itakuwa makao ya mbweha, mahali pa ukiwa milele. Hakuna yeyote atakayeishi humo; hakuna mtu atakayekaa ndani yake.” BIBLIA KISWAHILI Na Hazori utakuwa kao la mbwamwitu; ukiwa milele; hakuna mtu atakayekaa huko, wala hakuna mwanadamu atakayekaa huko kama mgeni akaavyo. |
Tena nitaifanya hiyo nchi kuwa makao ya nungunungu, na maziwa ya maji; nami nitaifagilia mbali kwa ufagio wa uharibifu; asema BWANA wa majeshi.
Sauti imesikiwa, Tazama, inakuja; mshindo mkuu kutoka nchi ya kaskazini, ili kuifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, makao ya mbweha.
Na Babeli utakuwa magofu, makao ya mbwamwitu, ajabu, na mazomeo, pasipo mtu wa kukaa huko.
Nami nitafanya Yerusalemu kuwa magofu, Makao ya mbweha; Nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, Isikaliwe na mtu awaye yote.
Basi kama niishivyo, asema BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, Hakika Moabu atakuwa kama Sodoma, na wana wa Amoni kama Gomora, yaani, milki ya upupu, na mashimo ya chumvi, ukiwa wa daima; watu wangu waliosalia watawateka nyara, na watu wa taifa langu waliobaki watawarithi.
bali Esau nimemchukia na kuifanya milima yake kuwa ukiwa, na urithi wake nimewapa mbweha wa nyikani.
Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ulio mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;