Akawaua Waedomi katika Bonde la Chumvi watu elfu kumi; akautwaa Sela vitani, akauita jina lake Yoktheeli hata leo.
Yeremia 49:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kuhusu kuogofya kwako, Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Ushikaye kilele cha milima; Ujapofanya kiota chako juu sana kama tai, Nitakushusha kutoka huko; asema BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Vitisho unavyotoa na kiburi chako vimekudanganya, ewe ukaaye katika mapango ya miamba, unayeishi juu ya kilele cha mlima! Ingawa unaweka makao yako juu kama ya tai, mimi nitakuporomosha kutoka huko uliko. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Biblia Habari Njema - BHND Vitisho unavyotoa na kiburi chako vimekudanganya, ewe ukaaye katika mapango ya miamba, unayeishi juu ya kilele cha mlima! Ingawa unaweka makao yako juu kama ya tai, mimi nitakuporomosha kutoka huko uliko. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Vitisho unavyotoa na kiburi chako vimekudanganya, ewe ukaaye katika mapango ya miamba, unayeishi juu ya kilele cha mlima! Ingawa unaweka makao yako juu kama ya tai, mimi nitakuporomosha kutoka huko uliko. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Neno: Bibilia Takatifu Vitisho vyako na kiburi cha moyo wako vimekudanganya, wewe unayeishi katika majabali ya miamba, wewe unayedumu katika miinuko ya kilima. Ujapojenga kiota chako juu sana kama cha tai, nitakushusha chini kutoka huko,” asema Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Vitisho vyako na kiburi cha moyo wako vimekudanganya, wewe unayeishi katika majabali ya miamba, wewe unayedumu katika miinuko ya kilima. Ujapojenga kiota chako juu sana kama cha tai, nitakushusha chini kutoka huko,” asema bwana. BIBLIA KISWAHILI Kuhusu kuogofya kwako, Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Ushikaye kilele cha milima; Ujapofanya kiota chako juu sana kama tai, Nitakushusha kutoka huko; asema BWANA. |
Akawaua Waedomi katika Bonde la Chumvi watu elfu kumi; akautwaa Sela vitani, akauita jina lake Yoktheeli hata leo.
Hua wangu, mafichoni mwa jabali, Katika sitara za, magenge Nitazame uso wako, nisikie sauti yako, Maana sauti yako ni tamu na uso wako unapendeza.
Na mkono wangu umezitoa mali za mataifa kama katika kiota cha ndege; na kama vile watu wakusanyavyo mayai yaliyoachwa, ndivyo nilivyokusanya dunia yote; wala hapana aliyetikisa bawa, wala kufumbua kinywa, wala kulia.
ili aingie ndani ya pango za majabali, na ndani ya tundu za miamba iliyopasuka, mbele za utisho wa BWANA na utukufu wa enzi yake, atakapoondoka ili aitetemeshe mno dunia.
Naam, BWANA asema hivi, Hata mateka wake aliye hodari watapokonywa mikononi mwake, na mateka wake aliye katili wataokoka; kwa maana nitapambana na yeye abishanaye nawe, nami nitawaletea wana wako wokovu.
Waiteni wapiga mishale juu ya Babeli, Naam, wote waupindao upinde; Pangeni hema kumzunguka pande zote; Ili asiokoke hata mtu mmoja wao; Mlipeni kwa kadiri ya kazi yake; Mtendeni sawasawa na yote aliyoyatenda; Kwa sababu amefanya kiburi juu ya BWANA, Juu yake aliye Mtakatifu wa Israeli.
Babeli ujapopanda mbinguni, na ujapopafanya mahali pa juu penye nguvu zake kuwa ngome, hata hivyo toka kwangu wenye kuangamiza watamwendea, asema BWANA.
Wajapochimba waingie katika kuzimu, mkono wangu utawatoa huko; nao wajapopanda hata mbinguni, nitawateremsha toka huko.
Ole wake yeye aipatiaye nyumba yake mapato mabaya, ili apate kukiweka kiota chake juu, apate kujiepusha na mkono wa uovu!
bali Esau nimemchukia na kuifanya milima yake kuwa ukiwa, na urithi wake nimewapa mbweha wa nyikani.