Na itakuwa atakayeokoka na upanga wa Hazaeli, Yehu atamwua; na atakayeokoka na upanga wa Yehu, Elisha atamwua.
Yeremia 48:44 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Aikimbiaye hofu ataanguka shimoni; na yeye atokaye shimoni atanaswa kwa mtego; maana nitaleta juu yake, yaani, juu ya Moabu, mwaka wa kujiliwa kwake, asema BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Atakayetoroka kitisho atatumbukia shimoni; atakayetoka shimoni atanaswa mtegoni. Kwa maana nitaleta mambo hayo juu ya Moabu, katika mwaka wao wa adhabu. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Atakayetoroka kitisho atatumbukia shimoni; atakayetoka shimoni atanaswa mtegoni. Kwa maana nitaleta mambo hayo juu ya Moabu, katika mwaka wao wa adhabu. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Atakayetoroka kitisho atatumbukia shimoni; atakayetoka shimoni atanaswa mtegoni. Kwa maana nitaleta mambo hayo juu ya Moabu, katika mwaka wao wa adhabu. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu “Yeyote atakayeikimbia hiyo hofu kuu ataanguka ndani ya shimo, yeyote atakayepanda kutoka shimoni, atanaswa katika mtego, kwa sababu nitailetea Moabu mwaka wa adhabu yake,” asema Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu “Yeyote atakayeikimbia hiyo hofu kuu ataanguka ndani ya shimo, yeyote atakayepanda kutoka shimoni, atanaswa katika mtego, kwa sababu nitaletea Moabu mwaka wa adhabu yake,” asema bwana. BIBLIA KISWAHILI Aikimbiaye hofu ataanguka shimoni; na yeye atokaye shimoni atanaswa kwa mtego; maana nitaleta juu yake, yaani, juu ya Moabu, mwaka wa kujiliwa kwake, asema BWANA. |
Na itakuwa atakayeokoka na upanga wa Hazaeli, Yehu atamwua; na atakayeokoka na upanga wa Yehu, Elisha atamwua.
Lakini waliosalia wakakimbia mpaka Afeki, mjini; na ukuta ukaanguka juu ya watu elfu ishirini na saba waliosalia. Ben-hadadi naye akakimbia, akaingia mjini, katika chumba cha ndani.
Nanyi mtafanya nini siku ya kujiliwa, na wakati wa uangamivu, utakaokuja kutoka mbali sana? Je! Mtamkimbilia nani mpate msaada? Na utukufu wenu mtauacha wapi?
Itakuwa kila akimbiaye sauti ya hofu ataanguka katika shimo; na kila apandaye na kutoka shimoni atanaswa na mtego; kwa maana madirisha yaliyo juu yamewekwa wazi, na misingi ya dunia inatikisika.
wala hapatakuwa na mtu atakayesalia kwao; maana nitaleta mabaya juu ya watu wa Anathothi, mwaka wa kujiliwa kwao.
Tazama, asema BWANA, Nitatuma watu kuwaita wavuvi wengi, nao watawavua; na baada ya hayo nitatuma watu kuwaita wawindaji wengi, nao watawawinda, watoke katika kila mlima, na kila kilima, na pango za majabali.
Kwa ajili ya hayo njia yao itakuwa kwao kama mahali pa kuteleza gizani; watateremshwa na kuanguka hapo; kwa maana nitaleta uovu juu yao, naam, mwaka wa kujiliwa kwao, asema BWANA.
Na askari wake waliojiwa, walio kati yake, Ni kama ndama walionona malishoni; Maana wao nao wamerudi nyuma, Wamekimbia wote pamoja, wasisimame; Maana siku ya msiba wao imewafikia, Wakati wa kujiliwa kwao.
Kimbieni, rudini nyuma, kaeni chini sana, enyi mnaokaa Dedani; maana nitaleta msiba wa Esau juu yake, wakati nitakapomwangalia.
Nimekutegea mtego, Ee Babeli, nawe ukanaswa, nawe ulikuwa huna habari; umeonekana, ukakamatwa, kwa sababu ulishindana na BWANA.
Wachinjeni mafahali wake wote; Na wateremkie machinjoni; Ole wao! Maana siku yao imewadia, Wakati wa kujiliwa kwao.
Je! Waliona aibu, walipokuwa wametenda machukizo? La! Hawakuona aibu kabisa, wala hawakuweza kuona haya usoni; basi wataanguka miongoni mwao waangukao; wakati wa kujiliwa kwao wataangushwa chini, asema BWANA.
Siku za kupatilizwa zimekuja, siku za kulipa zimefika; Israeli atayajua hayo; huyo nabii ni mpumbavu, huyo mtu mwenye roho ana wazimu; kwa sababu ya wingi wa uovu wako, na kwa sababu uadui umekuwa mkubwa.
Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma.
Mtu aliye mwema miongoni mwao ni kama mbigili; mtu aliye mwenye adili miongoni mwao ni mbaya kuliko boma la michongoma; hiyo siku ya walinzi wako, yaani, siku ya kujiliwa kwako, imefika; sasa kutatokea kufadhaika kwao.