Yeremia 48:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tumesikia habari za kiburi cha Moabu; Ya kuwa ana kiburi kingi; Ujeuri wake, na kiburi chake, na majivuno yake, Na jinsi alivyojitukuza moyoni mwake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu; Moabu ana majivuno sana. Tumesikia juu ya kujiona, kiburi na majivuno yake; tumesikia jinsi anavyojigamba moyoni. Biblia Habari Njema - BHND Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu; Moabu ana majivuno sana. Tumesikia juu ya kujiona, kiburi na majivuno yake; tumesikia jinsi anavyojigamba moyoni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu; Moabu ana majivuno sana. Tumesikia juu ya kujiona, kiburi na majivuno yake; tumesikia jinsi anavyojigamba moyoni. Neno: Bibilia Takatifu “Tumesikia kuhusu kiburi cha Moabu: kutakabari kwake kwa kiburi na majivuno, kiburi chake na ufidhuli wake, na kujivuna kwa moyo wake. Neno: Maandiko Matakatifu “Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu: kutakabari kwake kwa kiburi na majivuno, kiburi chake na ufidhuli wake, na kujivuna kwa moyo wake. BIBLIA KISWAHILI Tumesikia habari za kiburi cha Moabu; Ya kuwa ana kiburi kingi; Ujeuri wake, na kiburi chake, na majivuno yake, Na jinsi alivyojitukuza moyoni mwake. |
Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.
Mwenye kiburi na kutakabari, jina lake ni mbishi; Hutenda mambo katika majivuno ya kiburi chake.
Kumcha BWANA ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.
Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayashusha chini majivuno yao walio wakali;
Tumesikia habari za kiburi cha Moabu, ya kwamba ni mwenye kiburi kingi; habari za majivuno yake, na kiburi chake, na ghadhabu yake; majivuno yake si kitu.
Basi mimi, Nebukadneza, namhimidi Mfalme wa mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili.
Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.