Nitamtuma juu ya taifa lenye kukufuru, nitampa maagizo juu ya watu wa ghadhabu yangu, ateke nyara, na kuchukua mateka, na kuwakanyaga kama matope ya njiani.
Yeremia 47:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Utawezaje kutulia, Ikiwa BWANA amekupa agizo? Juu ya Ashkeloni na juu ya pwani, Ndipo alipoyaamuru hayo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini utawezaje kutulia, hali Mwenyezi-Mungu ameupa kazi? Ameuamuru ushambulie mji wa Ashkeloni na watu wanaoishi pwani.” Biblia Habari Njema - BHND Lakini utawezaje kutulia, hali Mwenyezi-Mungu ameupa kazi? Ameuamuru ushambulie mji wa Ashkeloni na watu wanaoishi pwani.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini utawezaje kutulia, hali Mwenyezi-Mungu ameupa kazi? Ameuamuru ushambulie mji wa Ashkeloni na watu wanaoishi pwani.” Neno: Bibilia Takatifu Lakini upanga utatuliaje wakati Mwenyezi Mungu ameuamuru, wakati ameuagiza kuishambulia Ashkeloni pamoja na pwani yake?” Neno: Maandiko Matakatifu Lakini upanga utatuliaje wakati bwana ameuamuru, wakati ameuagiza kuishambulia Ashkeloni pamoja na pwani yake?” BIBLIA KISWAHILI Utawezaje kutulia, Ikiwa BWANA amekupa agizo? Juu ya Ashkeloni na juu ya pwani, Ndipo alipoyaamuru hayo. |
Nitamtuma juu ya taifa lenye kukufuru, nitampa maagizo juu ya watu wa ghadhabu yangu, ateke nyara, na kuchukua mateka, na kuwakanyaga kama matope ya njiani.
Mimi mwenyewe nimewaamuru watu wangu waliowekwa wakfu kwangu, naam, nimewaita watu wangu walio hodari kwa ajili ya hasira yangu, watu wangu wenye kiburi.
Je! Hukusikia? Ni mimi niliyeyatenda hayo tokea zamani, na kuyafanya tokea siku za kale; nikayatimiza sasa, iwe kazi yako kuangamiza miji yenye boma, ibomoke na kuwa rundo la magofu.
Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya BWANA kwa ulegevu; na alaaniwe auzuiaye upanga wake usimwage damu.
Au nikileta upanga juu ya nchi ile, na kusema, Upanga, pita kati ya nchi hii, hata nikawakatilia mbali na nchi hiyo wanadamu na wanyama;
Basi, wewe mwanadamu, tabiri, ukapige makofi; upanga huo na uongezwe mara mbili, hata mara tatu; upanga wao waliotiwa jeraha kiasi cha kuwaua; ni upanga wa mkuu aliyetiwa jeraha kiasi cha kumwua; uwazungukao pande zote.
Uurudishe alani mwake. Mahali pale ulipoumbwa, katika nchi uliyozaliwa; nitakuhukumu wewe.
Mwanadamu, tabiri, useme, BWANA asema hivi; Nena, Upanga, upanga, umenolewa na kusuguliwa,
kwa sababu hiyo, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitanyosha mkono wangu juu ya Wafilisti, nami nitawakatilia mbali Wakerethi, na kuwaharibu wabakio pande za pwani.
Je! Tarumbeta itapigwa mjini, watu wasiogope? Mji utapatikana na hali mbaya, asiyoileta BWANA?
Sauti ya BWANA inaulilia mji, na mtu mwenye akili ataliona jina lako; isikieni hiyo fimbo na yeye aliyeiagiza.
Basi sasa nenda ukawapige Waamaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyonavyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, na mtoto anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda.