Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Yeremia 47:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Upaa umeupata Gaza; Ashkeloni umenyamazishwa Mabaki ya bonde lao; Hata lini utajikatakata?

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Watu wa Gaza wamenyoa upara kuomboleza; mji wa Ashkeloni umeangamia. Enyi watu wa Anakimu mliobaki mpaka lini mtajikatakata kwa huzuni?

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Watu wa Gaza wamenyoa upara kuomboleza; mji wa Ashkeloni umeangamia. Enyi watu wa Anakimu mliobaki mpaka lini mtajikatakata kwa huzuni?

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Watu wa Gaza wamenyoa upara kuomboleza; mji wa Ashkeloni umeangamia. Enyi watu wa Anakimu mliobaki mpaka lini mtajikatakata kwa huzuni?

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Gaza atanyoa kichwa chake katika kuomboleza, Ashkeloni atanyamazishwa. Enyi mabaki kwenye tambarare, mtajikatakata wenyewe hadi lini?

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Gaza atanyoa kichwa chake katika kuomboleza, Ashkeloni atanyamazishwa. Enyi mabaki kwenye tambarare, mtajikatakata wenyewe mpaka lini?

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Upaa umeupata Gaza; Ashkeloni umenyamazishwa Mabaki ya bonde lao; Hata lini utajikatakata?

Tazama sura
Tafsiri zingine



Yeremia 47:5
20 Marejeleo ya Msalaba  

Wakapiga kelele, wakajikatakata kwa visu na vyembe kama ilivyo desturi yao, hata damu ikawachuruzika.


Wanapanda juu hata Bayithi na Diboni, mpaka mahali palipo juu ili walie; juu ya Nebo na juu ya Medeba Wamoabi wanalia; Wana upaa juu ya vichwa vyao vyote; kila ndevu zimenyolewa.


Tena neno la BWANA likanijia, kusema,


Wakubwa kwa wadogo wote pia watakufa katika nchi hii; hawatazikwa, wala watu hawatawalilia, wala kujikatakata kwa ajili yao, wala kujinyoa kwa ajili yao;


na watu wote waliochanganyika pamoja, na wafalme wote wa nchi ya Uzi, na wafalme wote wa nchi ya Wafilisti, na Ashkeloni, na Gaza, na Ekroni, na mabaki ya Ashdodi;


wakafika watu kadhaa toka Shekemu, na toka Shilo, na toka Samaria, watu themanini, nao wamenyoa ndevu zao, na kurarua nguo zao, nao wamejikatakata, wakichukua sadaka na ubani mikononi mwao, ili wazilete nyumbani kwa BWANA.


Neno la BWANA lililomjia Yeremia, nabii, kuhusu Wafilisti, kabla Farao hajashambulia Gaza.


kwa sababu ya siku ijayo kuwaangamiza Wafilisti wote, kukatilia mbali kila msaidizi wa Tiro na Sidoni asaliaye; maana BWANA atawaharibu Wafilisti, mabaki ya kisiwa cha Kaftori.


Maana kila kichwa kina upara, na ndevu zote zimenyolewa; mikono yote ina alama za chale, na viuno vyote vimevikwa nguo za magunia.


kwa sababu hiyo, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitanyosha mkono wangu juu ya Wafilisti, nami nitawakatilia mbali Wakerethi, na kuwaharibu wabakio pande za pwani.


Tena watajifungia nguo za magunia, na utisho utawafunika; na aibu itakuwa juu ya nyuso zote, na upaa juu ya vichwa vyao vyote.


Msichanje chale yoyote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi BWANA.


Wasijifanyie upara kichwani, wala wasinyoe pembe za ndevu zao, wala wasichanje tojo katika miili yao.


Jinyoeni upara, jikateni nywele zenu, Kwa ajili ya watoto waliowafurahisha; Panueni upara wenu kama tai; Kwa maana wamekwenda mbali nanyi uhamishoni.


Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikatakata kwa mawe.


Ninyi mmekuwa wana wa BWANA, Mungu wenu; msijitoje miili yenu, wala msifanye upaa katikati ya macho yenu kwa ajili ya aliyekufa.


Pamoja na haya Yuda aliutwaa Gaza pamoja na mipaka yake, na Ashkeloni na mipaka yake, na Ekroni na mipaka yake.