Ee binti Babeli, uliye karibu na kuangamia, Heri atakayekupatiliza, ulivyotupatiliza sisi.
Yeremia 46:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Binti ya Misri ataaibishwa; Atatiwa mikononi mwa watu wa kaskazini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wa Misri wataaibishwa, watatiwa mikononi mwa watu kutoka kaskazini.” Biblia Habari Njema - BHND Watu wa Misri wataaibishwa, watatiwa mikononi mwa watu kutoka kaskazini.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wa Misri wataaibishwa, watatiwa mikononi mwa watu kutoka kaskazini.” Neno: Bibilia Takatifu Binti Misri ataaibishwa, atatiwa mikononi mwa watu wa kaskazini.” Neno: Maandiko Matakatifu Binti wa Misri ataaibishwa, atatiwa mikononi mwa watu wa kaskazini.” BIBLIA KISWAHILI Binti ya Misri ataaibishwa; Atatiwa mikononi mwa watu wa kaskazini. |
Ee binti Babeli, uliye karibu na kuangamia, Heri atakayekupatiliza, ulivyotupatiliza sisi.
Kwa kuwa, tazama, nitaziita jamaa zote za falme za kaskazini, asema BWANA; nao watakuja, na kuweka kila mtu kiti chake cha enzi mbele ya mahali pa kuingilia malango ya Yerusalemu, na kuzielekea kuta zake pande zote, na kuielekea miji yote ya Yuda.
Panda uende Gileadi, ukatwae zeri, Ee binti, bikira wa Misri; unatumia dawa nyingi bure tu; hupati kupona kamwe.
BWANA asema hivi, Tazama, maji yanatokea katika pande za kaskazini, nayo yatakuwa mto ufurikao, nayo yataifunika nchi, na kila kitu kilichomo, huo mji na wote wakaao ndani yake; nao watu watalia na watu wote wakaao katika nchi wataomboleza.