Basi mfalme wa Misri hakuja tena kutoka nchi yake; kwa kuwa mfalme wa Babeli alikuwa amemnyang'anya nchi, tangu kijito cha Misri mpaka mto wa Frati, yote aliyokuwa nayo mfalme wa Misri.
Yeremia 46:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana hiyo ni siku ya Bwana, BWANA wa majeshi, Siku ya kisasi, ili ajilipize kisasi juu ya adui zake; Nao upanga utakula na kushiba, Utakunywa damu yao hata kukinai; Maana Bwana, BWANA wa majeshi, ana sadaka yake Katika nchi ya kaskazini karibu na mto Frati. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Siku hiyo ni siku ya Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ni siku ya kulipiza kisasi; naam, siku ya kuwaadhibu maadui zake. Upanga utawamaliza hao na kutosheka, utainywa damu yao na kushiba. Maana Mwenyezi-Mungu wa majeshi anayo kafara huko kaskazini karibu na mto Eufrate. Biblia Habari Njema - BHND Siku hiyo ni siku ya Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ni siku ya kulipiza kisasi; naam, siku ya kuwaadhibu maadui zake. Upanga utawamaliza hao na kutosheka, utainywa damu yao na kushiba. Maana Mwenyezi-Mungu wa majeshi anayo kafara huko kaskazini karibu na mto Eufrate. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Siku hiyo ni siku ya Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ni siku ya kulipiza kisasi; naam, siku ya kuwaadhibu maadui zake. Upanga utawamaliza hao na kutosheka, utainywa damu yao na kushiba. Maana Mwenyezi-Mungu wa majeshi anayo kafara huko kaskazini karibu na mto Eufrate. Neno: Bibilia Takatifu Lakini ile siku ni ya Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, siku ya kulipiza kisasi, kisasi juu ya adui zake. Upanga utakula hata utakapotosheka, hadi utakapozima kiu yake kwa damu. Kwa maana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, atatoa dhabihu kwenye nchi ya kaskazini, kando ya Mto Frati. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini ile siku ni ya Bwana, bwana Mwenye Nguvu Zote, siku ya kulipiza kisasi, kisasi juu ya adui zake. Upanga utakula hata utakapotosheka, hadi utakapozima kiu yake kwa damu. Kwa maana Bwana, bwana Mwenye Nguvu Zote, atatoa dhabihu kwenye nchi ya kaskazini, kando ya Mto Frati. BIBLIA KISWAHILI Maana hiyo ni siku ya Bwana, BWANA wa majeshi, Siku ya kisasi, ili ajilipize kisasi juu ya adui zake; Nao upanga utakula na kushiba, Utakunywa damu yao hata kukinai; Maana Bwana, BWANA wa majeshi, ana sadaka yake Katika nchi ya kaskazini karibu na mto Frati. |
Basi mfalme wa Misri hakuja tena kutoka nchi yake; kwa kuwa mfalme wa Babeli alikuwa amemnyang'anya nchi, tangu kijito cha Misri mpaka mto wa Frati, yote aliyokuwa nayo mfalme wa Misri.
Pigeni kelele za hofu; maana siku ya BWANA i karibu; itanyesha kama maangamizi yatokayo kwa Mwenyezi Mungu.
Kwa maana kutakuwa siku ya BWANA wa majeshi juu ya watu wote wenye kiburi na majivuno, na juu ya yote yaliyoinuka; nayo yatashushwa chini.
Ndipo huyo Mwashuri ataanguka kwa upanga ambao si wa mtu; na upanga usio upanga wa mtu utamwangamiza; naye ataukimbia upanga, na vijana wake watatoa kodi.
Kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;
Watekao nyara wamepanda juu ya vilele vya milima katika nyika; kwa maana upanga wa BWANA utaangamiza toka upande mmoja wa nchi hata upande wa pili wa nchi; hapana mwenye mwili atakayekuwa na amani.
Tangazeni habari hii katika Misri, mkaihubiri katika Migdoli, na kuihubiri katika Nofu, na Tapanesi; semeni, Simama, ujitayarishe kwa maana upanga umekula pande zako zote.
Kuhusu Misri; habari za jeshi la Farao Neko, mfalme wa Misri, lililokuwa karibu na mto Frati katika Karkemishi, ambalo Nebukadneza, mfalme wa Babeli, alilipiga katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda.
Mtu mwepesi asikimbie, wala shujaa asiokoke; pande za kaskazini karibu na mto Frati wamejikwaa na kuanguka.
Mpigieni kelele pande zote; amejitoa; Maboma yake yameanguka, kuta zake zimebomolewa; Kwa maana ni kisasi cha BWANA; mlipizeni kisasi; Kama yeye alivyotenda, mtendeni yeye.
Basi, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, mimi nitamwadhibu mfalme wa Babeli, na nchi yake, kama nilivyomwadhibu mfalme wa Ashuru.
Kimbieni kutoka kati ya Babeli, kila mtu na ajiokoe nafsi yake; msikatiliwe mbali katika uovu wake; maana ni wakati wa kisasi cha BWANA, atamlipa malipo.
Nawe, mwanadamu, tabiri useme, Bwana MUNGU asema hivi, kuhusu wana wa Amoni, na kuhusu aibu yao; Nena, Upanga; upanga umefutwa; umeng'arishwa, ili kuua, ili kuufanya uue sana, upate kuwa kama umeme;
Ole wake siku hii! Kwa maana siku ya BWANA inakaribia, nayo itakuja kama maangamizi yatokayo kwake aliye Mwenyezi.
Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Pigeni na kelele katika mlima wangu mtakatifu; Wenyeji wote wa nchi na watetemeke; Kwa maana siku ya BWANA inakuja. Kwa sababu inakaribia;
Gari lile lenye farasi weusi latoka kwenda hata nchi ya kaskazini; nao farasi weupe wanatoka kwenda katika nchi ya magharibi; na wale wa rangi ya kijivujivu wakatoka kwenda hadi nchi ya kusini.
Nitailevya mishale yangu kwa damu, Na upanga wangu utakula nyama; Pamoja na damu ya waliouawa na waliotekwa nyara, Katika vichwa vya wakuu wa adui.