Wakaondoka watu wote, wadogo kwa wakubwa, pamoja na wakuu wa majeshi, wakainuka kwenda Misri; kwa kuwa waliwaogopa Wakaldayo.
Yeremia 43:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC wakaingia nchi ya Misri; maana hawakuitii sauti ya BWANA; wakafika hadi Tapanesi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema wakaenda nchini Misri, wakawasili mjini Tahpanesi. Ndivyo walivyokataa kutii alichosema Mwenyezi-Mungu Biblia Habari Njema - BHND wakaenda nchini Misri, wakawasili mjini Tahpanesi. Ndivyo walivyokataa kutii alichosema Mwenyezi-Mungu Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza wakaenda nchini Misri, wakawasili mjini Tahpanesi. Ndivyo walivyokataa kutii alichosema Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo wakaingia Misri kwa kutokumtii Mwenyezi Mungu, wakaenda hadi Tapanesi. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo wakaingia Misri kwa kutokumtii bwana, wakaenda mpaka Tahpanhesi. BIBLIA KISWAHILI wakaingia nchi ya Misri; maana hawakuitii sauti ya BWANA; wakafika hadi Tapanesi. |
Wakaondoka watu wote, wadogo kwa wakubwa, pamoja na wakuu wa majeshi, wakainuka kwenda Misri; kwa kuwa waliwaogopa Wakaldayo.
Ikawa, aliposema naye, mfalme akamwambia, Je! Tumekutia wewe kuwa mshauri wa mfalme? Nyamaza; kwa nini upigwe? Ndipo yule nabii akaacha, akasema, Najua ya kuwa Mungu amekusudia kukuangamiza, kwa sababu umeyafanya haya, wala hukulisikiliza shauri langu.
waendao kuteremkia Misri wala hawakuuliza kinywani mwangu; ili wajitie nguvu kwa nguvu za Farao, na kutumainia kivuli cha Misri.
wakaenda zao, wakakaa katika Geruthi Kimhamu, ulio karibu na Bethlehemu, ili wapate kuingia Misri,
nami nimewafunulia haya leo; lakini ninyi hamkuitii sauti ya BWANA, Mungu wenu, katika neno lolote ambalo amenituma kwenu.
Neno lililomjia Yeremia, kuhusu Wayahudi wote waliokaa katika nchi ya Misri, waliokaa Migdoli, na Tapanesi, na Nofu, na katika nchi ya Pathrosi, kusema,
Tena Yeremia akawaambia watu wote, na wanawake wote, Lisikieni neno hili la BWANA, ninyi nyote wa Yuda, mlioko hapa katika nchi ya Misri;
Tangazeni habari hii katika Misri, mkaihubiri katika Migdoli, na kuihubiri katika Nofu, na Tapanesi; semeni, Simama, ujitayarishe kwa maana upanga umekula pande zako zote.
Huko Tapanesi nako mchana utakuwa giza, nitakapovunja huko kongwa za Misri, na kiburi cha uwezo wake kitakoma ndani yake, na katika habari zake, wingu litaifunika, na binti zake watakwenda utumwani.