Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Yeremia 43:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Naye atakuja, na kuipiga nchi ya Misri; watu walioandikiwa kufa watakufa, nao walioandikiwa kuwa mateka watakuwa mateka, nao walioandikiwa kupigwa kwa upanga watapigwa kwa upanga.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Atakapofika ataiangamiza nchi ya Misri. Hapo waliopangiwa kufa kwa maradhi watakufa kwa maradhi, waliopangiwa kuchukuliwa mateka, watachukuliwa mateka; waliopangiwa kufia vitani watafia vitani.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Atakapofika ataiangamiza nchi ya Misri. Hapo waliopangiwa kufa kwa maradhi watakufa kwa maradhi, waliopangiwa kuchukuliwa mateka, watachukuliwa mateka; waliopangiwa kufia vitani watafia vitani.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Atakapofika ataiangamiza nchi ya Misri. Hapo waliopangiwa kufa kwa maradhi watakufa kwa maradhi, waliopangiwa kuchukuliwa mateka, watachukuliwa mateka; waliopangiwa kufia vitani watafia vitani.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Atakuja na kuishambulia Misri; atawaua waliokusudiwa kuuawa, atawateka waliokusudiwa kutekwa, na atawaua kwa upanga waliokusudiwa kuuawa kwa upanga.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Atakuja na kuishambulia Misri, akiwaua wale waliokusudiwa kuuawa, awateke mateka wale waliokusudiwa kutekwa, na upanga kwa wale waliokusudiwa upanga.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Naye atakuja, na kuipiga nchi ya Misri; watu walioandikiwa kufa watakufa, nao walioandikiwa kuwa mateka watakuwa mateka, nao walioandikiwa kupigwa kwa upanga watapigwa kwa upanga.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Yeremia 43:11
15 Marejeleo ya Msalaba  

Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu itokayo kwa Mungu, Na urithi aliowekewa na Mungu.

Kisha itakuwa, hapo watakapokuambia, Tutoke, tuende wapi? Utawaambia, BWANA asema hivi, Walioandikiwa kufa, watakwenda kufa; au kufa kwa upanga, watakufa kwa upanga; au kufa kwa njaa, watakufa kwa njaa, au kutekwa nyara, watakuwa mateka.

Maana BWANA, Mungu wa Israeli, aniambia hivi, Pokea kikombe cha divai ya ghadhabu hii mkononi mwangu, ukawanyweshe mataifa yote, ambao nitakupeleka kwao;

Farao, mfalme wa Misri, na watumishi wake na wakuu wake na watu wake wote;

Basi, sasa jueni sana ya kuwa mtakufa kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, katika mahali pale mnapopatamani kwenda na kukaa.

Nami nitawatwaa mabaki wa Yuda, walioelekeza nyuso zao kuiingia nchi ya Misri, wakae huko, nao wataangamia wote pia; wataanguka katika nchi ya Misri; wataangamia kwa upanga, na kwa njaa; watakufa, tangu wadogo hata wakubwa, kwa upanga, na kwa njaa; nao watakuwa apizo, na ajabu, na laana, na aibu.

Kwa maana nitawaadhibu wakaao katika nchi ya Misri, kama nilivyouadhibu Yerusalemu, kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni;

Hautapita kati yake mguu wa mwanadamu, wala hautapita kati yake mguu wa mnyama, wala haitakaliwa na watu, muda wa miaka arubaini.

Theluthi yenu mtakufa kwa tauni, na kwa njaa watakomeshwa ndani yako; na theluthi yenu wataanguka kwa upanga pande zako zote; na theluthi yenu nitawatawanya kwa pepo zote, kisha nitafuta upanga nyuma yao.

Ndipo nikasema, Sitawalisheni; afaye na afe; atakayekatiliwa mbali na akatiliwe mbali; nao waliosalia, kila mmoja na ale nyama ya mwili wa mwenziwe.

Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye subira na imani ya watakatifu.