Sikusitiri haki yako moyoni mwangu; Nimetangaza uaminifu wako na wokovu wako. Sikuficha fadhili zako wala kweli yako Katika kusanyiko kubwa.
Yeremia 42:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ndipo Yeremia, nabii, akawaambia, Nimewasikia; tazama, nitamwomba BWANA, Mungu wenu, sawasawa na maneno yenu; tena itakuwa, neno lolote ambalo BWANA atawajibu, nitawaambia; sitawazuilia neno liwalo lote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yeremia akawajibu, “Vema; nimesikia. Nitamwomba Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kama mlivyonisihi; jibu lolote atakalonipa Mwenyezi-Mungu, nitawaambieni; sitawaficha chochote.” Biblia Habari Njema - BHND Yeremia akawajibu, “Vema; nimesikia. Nitamwomba Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kama mlivyonisihi; jibu lolote atakalonipa Mwenyezi-Mungu, nitawaambieni; sitawaficha chochote.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yeremia akawajibu, “Vema; nimesikia. Nitamwomba Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kama mlivyonisihi; jibu lolote atakalonipa Mwenyezi-Mungu, nitawaambieni; sitawaficha chochote.” Neno: Bibilia Takatifu Nabii Yeremia akajibu, “Nimewasikia. Kwa hakika nitamwomba Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kama mlivyoomba. Nitawaambia kila kitu asemacho Mwenyezi Mungu, wala sitawaficha chochote.” Neno: Maandiko Matakatifu Nabii Yeremia akajibu, “Nimewasikia. Kwa hakika nitamwomba bwana Mwenyezi Mungu wenu kama mlivyoomba. Nitawaambia kila kitu asemacho bwana, wala sitawaficha chochote.” BIBLIA KISWAHILI Ndipo Yeremia, nabii, akawaambia, Nimewasikia; tazama, nitamwomba BWANA, Mungu wenu, sawasawa na maneno yenu; tena itakuwa, neno lolote ambalo BWANA atawajibu, nitawaambia; sitawazuilia neno liwalo lote. |
Sikusitiri haki yako moyoni mwangu; Nimetangaza uaminifu wako na wokovu wako. Sikuficha fadhili zako wala kweli yako Katika kusanyiko kubwa.
Musa akasema, Tazama, mimi natoka kwako, nami nitamwomba BWANA ili hao inzi wamtoke Farao, na watumishi wake, na watu wake kesho; lakini Farao asitende kwa udanganyifu tena, kwa kutowaacha watu waende kumchinjia BWANA dhabihu.
Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na neno langu, na aseme neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema BWANA.
Mtasema hivi kila mtu na jirani yake, na kila mtu na ndugu yake, BWANA amejibu mtu? Na, BWANA amesemaje?
BWANA asema hivi, Simama katika uwanja wa nyumba ya BWANA, useme na miji yote ya Yuda, wajao ili kuabudu katika nyumba ya BWANA; sema nao maneno yote ninayokuamuru kuwaambia, usizuie hata neno moja.
Nawe utawaambia maneno yangu, iwe watasikia au hawataki kusikia; maana hao wanaasi sana.
ya kuwa sikujiepusha katika kuwatangazia neno lolote liwezalo kuwafaa bali niliwafundisha waziwazi, na nyumba kwa nyumba,
Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe.
Lakini mimi, hasha! Nisimtende BWANA dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka