Yeremia 42:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana mmetenda kwa hila juu ya nafsi zenu wenyewe; kwa kuwa mmenituma kwa BWANA, Mungu wenu, mkisema, Utuombee kwa BWANA, Mungu wetu, ukatufunulie sawasawa na yote atakayoyanena BWANA, Mungu wetu, nasi tutayatenda; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema mmepotoka, mmeyahatarisha maisha yenu. Maana mlinituma kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mkiniambia, ‘Tuombee dua kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, na chochote Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu atakachosema, utuambie, nasi tutatekeleza.’ Biblia Habari Njema - BHND mmepotoka, mmeyahatarisha maisha yenu. Maana mlinituma kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mkiniambia, ‘Tuombee dua kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, na chochote Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu atakachosema, utuambie, nasi tutatekeleza.’ Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza mmepotoka, mmeyahatarisha maisha yenu. Maana mlinituma kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mkiniambia, ‘Tuombee dua kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, na chochote Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu atakachosema, utuambie, nasi tutatekeleza.’ Neno: Bibilia Takatifu kwamba mmefanya kosa kubwa mioyoni mwenu mliponituma kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, na kusema, ‘Mwombe Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, kwa ajili yetu, nawe utuambie kila kitu atakachosema, nasi tutafanya.’ Neno: Maandiko Matakatifu kwamba mmefanya kosa kubwa mioyoni mwenu mliponituma kwa bwana Mwenyezi Mungu wenu na kusema, ‘Mwombe bwana Mwenyezi Mungu wetu kwa ajili yetu, nawe utuambie kila kitu atakachosema, nasi tutafanya.’ BIBLIA KISWAHILI Maana mmetenda kwa hila juu ya nafsi zenu wenyewe; kwa kuwa mmenituma kwa BWANA, Mungu wenu, mkisema, Utuombee kwa BWANA, Mungu wetu, ukatufunulie sawasawa na yote atakayoyanena BWANA, Mungu wetu, nasi tutayatenda; |
Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.
Na pamoja na hayo yote dada yake, Yuda mwenye hiana, hajanirudia mimi kwa moyo wake wote, bali kwa unafiki, asema BWANA.
Sedekia, mfalme, akamtuma Yehukali, mwana wa Shelemia, na Sefania, mwana wa Maaseya, kuhani, kwa Yeremia, nabii, kusema, Utuombee sasa kwa BWANA, Mungu wetu.
Kisha mfalme Sedekia akatuma watu, akamleta nabii Yeremia kwake, ndani ya maingilio ya tatu ya nyumba ya BWANA; mfalme akamwambia Yeremia, Nataka kukuuliza neno, nawe usinifiche neno lolote.
wakamwambia Yeremia, nabii, Twakusihi, maombi yetu yakubaliwe mbele yako, ukatuombee kwa BWANA, Mungu wako, yaani, watu hawa wote waliosalia; maana tumesalia wachache tu katika watu wengi, kama macho yako yatuonavyo;
Wakamwambia Yeremia, BWANA na awe shahidi wa kweli na uaminifu kati yetu; ikiwa hatufanyi sawasawa na neno lile, ambalo BWANA, Mungu wako, atakutuma utuletee.
ndipo Azaria, mwana wa Hoshaya, na Yohana mwana wa Karea, na watu wote wenye kiburi wakanena, wakimwambia Yeremia, Unasema uongo; BWANA, Mungu wetu, hakukutuma useme, Msiende Misri kukaa huko;
Nao huja kwako kama watu wajavyo, nao hukaa mbele yako kama watu wangu, nao husikia maneno yako, wasiyatende; maana kwa vinywa vyao hujifanya kuwa wenye upendo mwingi, lakini mioyo yao inatafuta faida yao.
vile vyetezo vya hao waliofanya dhambi na kuziumiza nafsi zao wenyewe, na vifanywe mbao za kufuliwa kuwa kifuniko cha madhabahu; kwa kuwa walivisongeza mbele za BWANA, navyo ni vitakatifu; vitakuwa ishara kwa wana wa Israeli.
Na katika fimbo ya Lawi utaliandika jina la Haruni; maana, itakuwa fimbo moja kwa kila kichwa cha nyumba za baba zao.