Lakini ikawa katika mwezi wa saba Ishmaeli mwana wa Nethania, mwana wa Elishama, mmoja wa wazao wa kifalme, na watu kumi pamoja naye, wakamwendea Gedalia, wakampiga hata akafa, na hao Wayahudi na Wakaldayo waliokuwa pamoja naye huko Mispa.
Yeremia 41:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tena Ishmaeli akawaua Wayahudi wote waliokuwa pamoja naye, yaani, pamoja na Gedalia, huko Mizpa, na hao Wakaldayo walioonekana huko, yaani, watu wa vita. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ishmaeli aliwaua pia Wayahudi wote waliokuwa pamoja na Gedalia huko Mizpa na wanajeshi Wakaldayo waliokuwa mahali hapo. Biblia Habari Njema - BHND Ishmaeli aliwaua pia Wayahudi wote waliokuwa pamoja na Gedalia huko Mizpa na wanajeshi Wakaldayo waliokuwa mahali hapo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ishmaeli aliwaua pia Wayahudi wote waliokuwa pamoja na Gedalia huko Mizpa na wanajeshi Wakaldayo waliokuwa mahali hapo. Neno: Bibilia Takatifu Ishmaeli akawaua pia Wayahudi wote waliokuwa na Gedalia huko Mispa, pamoja na askari Wakaldayo waliokuwa huko. Neno: Maandiko Matakatifu Ishmaeli akawaua pia Wayahudi wote waliokuwa na Gedalia huko Mispa, pamoja na askari wa Kikaldayo waliokuwa huko. BIBLIA KISWAHILI Tena Ishmaeli akawaua Wayahudi wote waliokuwa pamoja naye, yaani, pamoja na Gedalia, huko Mizpa, na hao Wakaldayo walioonekana huko, yaani, watu wa vita. |
Lakini ikawa katika mwezi wa saba Ishmaeli mwana wa Nethania, mwana wa Elishama, mmoja wa wazao wa kifalme, na watu kumi pamoja naye, wakamwendea Gedalia, wakampiga hata akafa, na hao Wayahudi na Wakaldayo waliokuwa pamoja naye huko Mispa.
Akaondoka huyo Ishmaeli, mwana wa Nethania, na watu wale kumi waliokuwa pamoja naye, wakampiga Gedalia, mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, kwa upanga, wakamwua; yeye ambaye mfalme wa Babeli amemweka kuwa mtawala wa nchi.
Hulia sana wakati wa usiku, Na machozi yake yapo mashavuni; Miongoni mwa wote waliompenda Hakuna hata mmoja amfarijiye; Rafiki zake wote wamemtenda hila, Wamekuwa adui zake.