Katika mwaka wa thelathini na sita wa kutawala kwake Asa, Baasha mfalme wa Israeli alipanda juu ya Yuda, akaujenga Rama, ili asimwache mtu yeyote kutoka wala kuingia kwa Asa mfalme wa Yuda.
Yeremia 40:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa BWANA, baada ya wakati ule Nebuzaradani, mkuu wa askari walinzi, alipomwacha aende zake toka Rama, baada ya kumchukua akiwa amefungwa minyororo, pamoja na wafungwa wote wa Yerusalemu na Yuda, waliochukuliwa wakiwa wamefungwa mpaka Babeli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Mwenyezi-Mungu wakati Nebuzaradani kapteni wa walinzi wa mfalme, alipomruhusu Yeremia aondoke Rama. Huyo kapteni alimchukua Yeremia amefungwa minyororo, akawachukua pia pamoja naye mateka wengine wote wa Yerusalemu na Yuda ambao walikuwa wamepelekwa uhamishoni Babuloni. Biblia Habari Njema - BHND Neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Mwenyezi-Mungu wakati Nebuzaradani kapteni wa walinzi wa mfalme, alipomruhusu Yeremia aondoke Rama. Huyo kapteni alimchukua Yeremia amefungwa minyororo, akawachukua pia pamoja naye mateka wengine wote wa Yerusalemu na Yuda ambao walikuwa wamepelekwa uhamishoni Babuloni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Mwenyezi-Mungu wakati Nebuzaradani kapteni wa walinzi wa mfalme, alipomruhusu Yeremia aondoke Rama. Huyo kapteni alimchukua Yeremia amefungwa minyororo, akawachukua pia pamoja naye mateka wengine wote wa Yerusalemu na Yuda ambao walikuwa wamepelekwa uhamishoni Babuloni. Neno: Bibilia Takatifu Neno likamjia Yeremia kutoka kwa Mwenyezi Mungu baada ya Nebuzaradani mkuu wa askari walinzi wa mfalme kumfungua huko Rama. Alikuwa amemkuta Yeremia akiwa amefungwa kwa minyororo miongoni mwa mateka wote kutoka Yerusalemu na Yuda waliokuwa wakipelekwa uhamishoni Babeli. Neno: Maandiko Matakatifu Neno likamjia Yeremia kutoka kwa bwana baada ya Nebuzaradani kiongozi wa walinzi wa mfalme kumfungua huko Rama. Alikuwa amemkuta Yeremia akiwa amefungwa kwa minyororo miongoni mwa mateka wote kutoka Yerusalemu na Yuda waliokuwa wakipelekwa uhamishoni Babeli. BIBLIA KISWAHILI Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa BWANA, baada ya wakati ule Nebuzaradani, mkuu wa askari walinzi, alipomwacha aende zake toka Rama, baada ya kumchukua akiwa amefungwa minyororo, pamoja na wafungwa wote wa Yerusalemu na Yuda, waliochukuliwa wakiwa wamefungwa mpaka Babeli. |
Katika mwaka wa thelathini na sita wa kutawala kwake Asa, Baasha mfalme wa Israeli alipanda juu ya Yuda, akaujenga Rama, ili asimwache mtu yeyote kutoka wala kuingia kwa Asa mfalme wa Yuda.
Mungu huwapa wapweke makao yao; Huwapa wafungwa uhuru na kuwafanikisha; Bali wakaidi huishi katika nchi kavu.
BWANA asema hivi, Sauti imesikiwa Rama, kilio, na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake; asikubali kufarijiwa kwa watoto wake, kwa kuwa hawako.
Basi, Nebuzaradani, mkuu wa askari walinzi, akawachukua mateka mabaki ya watu waliosalia katika mji mpaka Babeli, na hao pia waliouacha mji na kujiunga naye, na mabaki ya watu waliosalia.
Ikawa, katika mwaka wa kumi na mbili wa kuhamishwa kwetu, mwezi wa kumi, siku ya tano ya mwezi, mtu mmoja aliyekuwa ametoroka toka Yerusalemu akanijia, akisema, Mji umetekwa.
Ndipo Paulo alipojibu, Mnafanya nini, kulia na kunivunja moyo? Kwa maana mimi, licha ya kufungwa, ni tayari hata kuuawa katika Yerusalemu kwa ajili ya jina lake Bwana Yesu.
Basi kwa ajili ya hayo, nimewaita mje kunitazama na kusema nami; kwa maana nimefungwa kwa mnyororo huu kwa ajili ya tumaini la Israeli.
ambayo kwa ajili yake mimi ni mjumbe katika minyororo; hata nipate ujasiri katika huyo kunena jinsi inipasavyo kunena.
Kisha alikuwa akirudi Rama; maana ndipo ilipokuwa nyumba yake; nako ndiko alikowaamua Waisraeli; na huko akamjengea BWANA madhabahu.