Hata lini itaomboleza nchi, na kukauka majani ya nchi yote? Kwa ajili ya mabaya yao wakaao ndani yake, wanyama wameangamia na ndege pia; kwa sababu walisema, Yu kipofu katika njia zetu.
Yeremia 4:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nikaangalia, na tazama, hapakuwa na mtu hata mmoja, na ndege wote wa angani wamekwenda zao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nilikodoa macho wala sikuona mtu; hata ndege angani walikuwa wametoweka. Biblia Habari Njema - BHND Nilikodoa macho wala sikuona mtu; hata ndege angani walikuwa wametoweka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nilikodoa macho wala sikuona mtu; hata ndege angani walikuwa wametoweka. Neno: Bibilia Takatifu Nilitazama, wala hapakuwa na watu; kila ndege wa angani alikuwa ameruka zake. Neno: Maandiko Matakatifu Nilitazama, wala watu hawakuwepo; kila ndege wa angani alikuwa ameruka zake. BIBLIA KISWAHILI Nikaangalia, na tazama, hapakuwa na mtu hata mmoja, na ndege wote wa angani wamekwenda zao. |
Hata lini itaomboleza nchi, na kukauka majani ya nchi yote? Kwa ajili ya mabaya yao wakaao ndani yake, wanyama wameangamia na ndege pia; kwa sababu walisema, Yu kipofu katika njia zetu.
Kwa milima nitalia na kulalama, Na kwa malisho ya nyikani nitafanya maombolezo; Kwa sababu yameteketea, hata hakuna apitaye, Wala hapana awezaye kusikia sauti ya ng'ombe; Ndege wa angani, na wanyama wa mwituni, Wamekimbia, wamekwenda zao.
Je! Nisiwaadhibu kwa mambo hayo? Asema BWANA; na nafsi yangu je! Nisijilipize kisasi juu ya taifa la namna hii?
hata samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama wa mwituni, na vitu vyote vitambaavyo juu ya nchi, na wanadamu wote walio juu ya uso wa nchi, watatetemeka mbele ya uso wangu; nayo milima itatupwa chini, na magenge yataanguka, na kila ukuta utaanguka chini.
Kwa ajili ya hayo nchi itaomboleza, na kila mtu akaaye ndani yake atadhoofika, pamoja na wanyama wa porini na ndege wa angani; naam, samaki wa baharini pia wataangamizwa.