Karibuni, enyi mataifa, mpate kusikia; sikilizeni, enyi makabila ya watu; dunia na isikie, na chote kiijazacho, ulimwengu na vitu vyote viutokavyo.
Yeremia 4:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wapasheni mataifa habari; angalieni, hubirini juu ya Yerusalemu, ya kwamba walinzi wanatoka katika nchi ya mbali, wanatoa sauti yao juu ya miji ya Yuda. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Inayaonya mataifa, inaitangazia Yerusalemu: “Wavamizi waja kutoka nchi ya mbali, wanaitisha miji ya Yuda, Biblia Habari Njema - BHND Inayaonya mataifa, inaitangazia Yerusalemu: “Wavamizi waja kutoka nchi ya mbali, wanaitisha miji ya Yuda, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Inayaonya mataifa, inaitangazia Yerusalemu: “Wavamizi waja kutoka nchi ya mbali, wanaitisha miji ya Yuda, Neno: Bibilia Takatifu “Waambie mataifa jambo hili, piga mbiu hii dhidi ya Yerusalemu: ‘Jeshi la kuzingira linakuja kutoka nchi ya mbali, likipiga kelele za vita dhidi ya miji ya Yuda. Neno: Maandiko Matakatifu “Waambie mataifa jambo hili, piga mbiu hii dhidi ya Yerusalemu: ‘Jeshi la kuzingira linakuja kutoka nchi ya mbali, likipiga kelele ya vita dhidi ya miji ya Yuda. BIBLIA KISWAHILI Wapasheni mataifa habari; angalieni, hubirini juu ya Yerusalemu, ya kwamba walinzi wanatoka katika nchi ya mbali, wanatoa sauti yao juu ya miji ya Yuda. |
Karibuni, enyi mataifa, mpate kusikia; sikilizeni, enyi makabila ya watu; dunia na isikie, na chote kiijazacho, ulimwengu na vitu vyote viutokavyo.
Ndipo Isaya nabii akamwendea mfalme Hezekia, akamwambia, Watu hawa walisema nini? Nao wametoka wapi kuja kwako? Hezekia akasema, Wametoka katika nchi iliyo mbali, wakaja kwangu toka Babeli.
Kwa kuwa, tazama, nitaziita jamaa zote za falme za kaskazini, asema BWANA; nao watakuja, na kuweka kila mtu kiti chake cha enzi mbele ya mahali pa kuingilia malango ya Yerusalemu, na kuzielekea kuta zake pande zote, na kuielekea miji yote ya Yuda.
Wakubwa kwa wadogo wote pia watakufa katika nchi hii; hawatazikwa, wala watu hawatawalilia, wala kujikatakata kwa ajili yao, wala kujinyoa kwa ajili yao;
Wanasimba wamenguruma juu yake, wametoa sana sauti zao; Nao wameifanya nchi yake kuwa ukiwa; miji yake imeteketea, haina watu.
Lisikieni neno la BWANA, enyi mataifa, litangazeni visiwani mbali; mkaseme, Aliyemtawanya Israeli atamkusanya, na kumlinda, kama mchungaji alindavyo kundi lake.
Hata ikawa, Yerusalemu ulipotwaliwa, (katika mwaka wa tisa wa Sedekia, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi, Nebukadneza, mfalme wa Babeli, na jeshi lake lote, wakaja juu ya Yerusalemu, wakauzingira;
Kama watu walindao shamba, wameuzunguka wauhusuru; kwa sababu ameniasi mimi, asema BWANA.
Angalia, nitaleta taifa juu yenu litokalo mbali sana, Ee nyumba ya Israeli, asema BWANA; ni taifa hodari, ni taifa la zamani sana, taifa ambalo hujui lugha yake, wala huyafahamu wasemayo.
Basi, kwa hiyo, simba atokaye mwituni atawaua, mbwamwitu wa jioni atawateka, chui ataivizia miji yao, kila mtu atokaye humo atararuliwa vipande vipande; kwa sababu makosa yao ni mengi, na kurudi nyuma kwao kumezidi.
Tangazeni katika mataifa, Mkahubiri na kutweka bendera; Hubirini, msifiche, semeni, Babeli umetwaliwa! Beli amefedheheka; Merodaki amefadhaika; Sanamu zake zimeaibishwa, Vinyago vyake vimefadhaika.
Kwa sababu hiyo sikilizeni, enyi mataifa, mkajue, Ee kusanyiko, ni jambo gani litokealo kati yao.
Sikia, Ee nchi; tazama, nitaleta mabaya juu ya watu hawa, naam, matunda ya mawazo yao, kwa sababu hawakuyasikiliza maneno yangu; tena kwa habari ya sheria yangu, wameikataa.
BWANA asema hivi, Tazama, watu wanakuja, wakitoka katika nchi ya kaskazini; na taifa kubwa litaamshwa, litokalo katika pande za mwisho wa dunia.
Washika upinde na mkuki; ni wakatili, hawana huruma; sauti yao huvuma kama bahari, nao wamepanda farasi wao; kila mmoja kama mtu wa vita amejipanga juu yako, Ee binti Sayuni.
Tazama, sauti ya kilio cha binti ya watu wangu, itokayo katika nchi iliyo mbali sana; Je! BWANA hayumo katika Sayuni? Mfalme wake hayumo ndani yake? Mbona wamenikasirisha kwa sanamu zao walizochonga, na kwa ubatili wa kigeni?
Katika mkono wake wa kulia alikuwa na kura ya Yerusalemu, kuviweka vyombo vya kubomolea, kufumbua kinywa katika machinjo, kuiinua sauti kwa kupiga kelele sana, kuweka vyombo vya kubomolea juu ya malango, kufanya maboma, na kujenga ngome.