Yeremia 39:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mtwae, umtunze sana, wala usimtende neno baya lolote; lakini umtendee kama atakavyokuambia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Mchukue Yeremia, umtunze vema wala usimdhuru; mtendee kama anavyokuambia.” Biblia Habari Njema - BHND “Mchukue Yeremia, umtunze vema wala usimdhuru; mtendee kama anavyokuambia.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Mchukue Yeremia, umtunze vema wala usimdhuru; mtendee kama anavyokuambia.” Neno: Bibilia Takatifu “Mchukue umtunze. Usimdhuru, lakini umfanyie chochote anachotaka.” Neno: Maandiko Matakatifu “Mchukue umtunze. Usimdhuru, lakini umfanyie chochote anachotaka.” BIBLIA KISWAHILI Mtwae, umtunze sana, wala usimtende neno baya lolote; lakini umtendee kama atakavyokuambia. |
Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa BWANA; Kama mifereji ya maji huugeuza popote apendapo.
Je! Utavikazia macho vile ambavyo si kitu? Maana bila shaka mali hujifanyia mabawa, Kama tai arukaye mbinguni.
BWANA akasema, Hakika nitakutia nguvu upate mema; hakika nitamlazimisha adui akusihi wakati wa uovu, na wakati wa taabu.
Nami nitakuokoa kutoka kwa mkono wa watu wabaya, nami nitakukomboa kutoka kwa mkono wao wenye kutisha.
Kwa maana nitawaelekezea macho yangu, wapate mema, nami nitawaingiza katika nchi hii tena; nami nitawajenga, wala sitawabomoa; nitawapanda wala sitawang'oa.
Basi Nebuzaradani, mkuu wa askari walinzi, na Nebu-Shazbani, mkuu wa matowashi, na Nergal-Shareza, mkuu wa wanajimu, na maofisa wote wakuu wa mfalme wa Babeli,
Na sasa, tazama, nakufungulia leo minyororo hii iliyo mikononi mwako. Kama ukiona ni vema kwenda Babeli pamoja nami, haya! Njoo, nami nitakutunza sana; lakini kama ukiona ni vibaya kwenda Babeli pamoja nami, basi, acha; tazama, nchi yote iko mbele yako; palipo pema machoni pako na pa kukufaa, nenda huko.
Nao wajapokwenda kuwa mateka mbele ya adui zao, nitauagiza upanga huko, nao utawaua; nami nitawaelekezea macho yangu niwatende mabaya, wala si mema.
akamtoa katika dhiki zake zote, akampa fadhili na hekima mbele ya Farao, mfalme wa Misri; naye akamfanya awe mtawala juu ya Misri na nyumba yake yote.