Na Yekonia, mfalme wa Yuda, akatoka akamwendea mfalme wa Babeli, yeye na mama yake, na watumishi wake, na wakuu wa watu wake, na maofisa wake; mfalme wa Babeli akamchukua mateka katika mwaka wa nane wa kutawala kwake.
Yeremia 37:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na Sedekia, mwana wa Yosia, akamiliki baada ya Konia, mwana wa Yehoyakimu, ambaye Nebukadneza amemfanya mtawala katika nchi ya Yuda. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mfalme Nebukadneza wa Babuloni alimtawaza Sedekia mwana wa Yosia, kuwa mfalme wa Yuda mahali pa Konia mwana wa Yehoyakimu. Biblia Habari Njema - BHND Mfalme Nebukadneza wa Babuloni alimtawaza Sedekia mwana wa Yosia, kuwa mfalme wa Yuda mahali pa Konia mwana wa Yehoyakimu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mfalme Nebukadneza wa Babuloni alimtawaza Sedekia mwana wa Yosia, kuwa mfalme wa Yuda mahali pa Konia mwana wa Yehoyakimu. Neno: Bibilia Takatifu Sedekia mwana wa Yosia akafanywa kuwa mfalme wa Yuda na Nebukadneza mfalme wa Babeli, naye akatawala mahali pa Yehoyakini mwana wa Yehoyakimu. Neno: Maandiko Matakatifu Sedekia mwana wa Yosia akafanywa kuwa mfalme wa Yuda na Nebukadneza mfalme wa Babeli, naye akatawala mahali pa Yehoyakini mwana wa Yehoyakimu. BIBLIA KISWAHILI Na Sedekia, mwana wa Yosia, akamiliki baada ya Konia, mwana wa Yehoyakimu, ambaye Nebukadneza amemfanya mtawala katika nchi ya Yuda. |
Na Yekonia, mfalme wa Yuda, akatoka akamwendea mfalme wa Babeli, yeye na mama yake, na watumishi wake, na wakuu wa watu wake, na maofisa wake; mfalme wa Babeli akamchukua mateka katika mwaka wa nane wa kutawala kwake.
Mfalme wa Babeli akamtawaza Matania, ndugu ya baba yake, awe mfalme badala yake, akalibadili jina lake, akamwita Sedekia.
Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa BWANA, hapo mfalme Sedekia alipomtuma Pashuri, mwana wa Malkiya, na Sefania, mwana wa Maaseya, kuhani, kusema,
Kama niishivyo mimi, asema BWANA, hata Konia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, angekuwa pete yenye mhuri katika mkono wangu wa kulia, ningekung'oa wewe hapo;
Je! Mtu huyu, Konia, ni chombo kilichodharauliwa, na kuvunjika? Ni chombo kisichopendeza? Mbona wametupwa, yeye na wazao wake, na kutupwa katika nchi wasiyoijua?
BWANA akanionesha, na tazama, vikapu viwili vya tini, vimewekwa mbele ya hekalu la BWANA, baada ya Nebukadneza, mfalme wa Babeli, kumchukua mateka Yekonia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, na wakuu wa Yuda, pamoja na mafundi na wafua chuma, kutoka Yerusalemu, kuwaleta Babeli.
BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nenda ukaseme na Sedekia, mfalme wa Yuda, ukamwambie, BWANA asema hivi, Tazama, nitatia mji huu katika mikono ya mfalme wa Babeli, naye atauteketeza kwa moto;
Hata ikawa, katika mwaka wa thelathini na saba wa kuhamishwa kwake Yehoyakini, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya ishirini na tano ya mwezi, Evil-merodaki, mfalme wa Babeli, katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, akamwinua kichwa chake Yehoyakini, mfalme wa Yuda, akamtoa gerezani.