Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Yeremia 34:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

wakuu wa Yuda, na wakuu wa Yerusalemu, matowashi, na makuhani, na watu wote wa nchi, waliopita katikati ya vipande vile vya huyo ndama;

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Watu hao ndio hao maofisa wa Yuda, maofisa wa mji wa Yerusalemu, matowashi, makuhani, pamoja na wananchi wote waliopita katikati ya sehemu mbili za yule ndama.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Watu hao ndio hao maofisa wa Yuda, maofisa wa mji wa Yerusalemu, matowashi, makuhani, pamoja na wananchi wote waliopita katikati ya sehemu mbili za yule ndama.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Watu hao ndio hao maofisa wa Yuda, maofisa wa mji wa Yerusalemu, matowashi, makuhani, pamoja na wananchi wote waliopita katikati ya sehemu mbili za yule ndama.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Viongozi wa Yuda na Yerusalemu, maafisa wa mahakama, makuhani na watu wote wa nchi waliopita kati ya vile vipande vya ndama,

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Viongozi wa Yuda na Yerusalemu, maafisa wa mahakama, makuhani na watu wote wa nchi waliopita kati ya vile vipande vya ndama,

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

wakuu wa Yuda, na wakuu wa Yerusalemu, matowashi, na makuhani, na watu wote wa nchi, waliopita katikati ya vipande vile vya huyo ndama;

Tazama sura
Tafsiri zingine

Yeremia 34:19
14 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa, jua lilipokuchwa likawa giza, tazama, tanuri ya moshi na mwenge unaowaka ulipita kati ya vile vipande vya nyama.

Akasema, Ee Bwana MUNGU, nipateje kujua ya kwamba nitaimiliki?

Na Yekonia, mfalme wa Yuda, akatoka akamwendea mfalme wa Babeli, yeye na mama yake, na watumishi wake, na wakuu wa watu wake, na maofisa wake; mfalme wa Babeli akamchukua mateka katika mwaka wa nane wa kutawala kwake.

Akamchukua Yekonia mpaka Babeli; na mama yake mfalme, na wake zake mfalme, na maofisa wake, na wakuu wa nchi, aliwachukua mateka toka Yerusalemu mpaka Babeli.

(hapo walipokwisha kutoka Yerusalemu Yekonia mfalme, na mama yake mfalme, na matowashi, na wakuu wa Yuda na Yerusalemu, na mafundi, na wahunzi;)

na wakuu wote, na watu wote, wakati, waliofanya agano hilo, ya kwamba kila mtu amweke huru mtumwa wake na mjakazi wake, mtu yeyote asiwatumikishe tena; wakatii, wakawaacha.

Basi, Ebedmeleki, Mkushi, towashi, aliyekuwa katika nyumba ya mfalme, aliposikia kwamba wamemtia Yeremia shimoni; na wakati huo mfalme alikuwa amekaa katika lango la Benyamini;

Ndipo mfalme wa Babeli akawaua wana wa Sedekia huko Ribla mbele ya macho yake; pia mfalme wa Babeli akawaua wakuu wote wa Yuda.

Naye ameyathibitisha maneno yake, aliyoyanena juu yetu, na juu ya waamuzi wetu waliotuamua, kwa kumletea mambo maovu makuu; maana chini ya mbingu zote halikutendeka jambo kama hili, lilivyotendeka juu ya Yerusalemu.

wala hatukuwasikiliza watumishi wako, manabii, ambao kwa jina lako walisema na wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, na watu wote wa nchi.

Ee Bwana, kwetu sisi kuna aibu, kwa wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, kwa sababu tumekutenda dhambi.