Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Yeremia 30:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Maana BWANA asema hivi, Tumesikia sauti ya tetemeko, na ya hofu, wala si ya amani.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

“Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Kumesikika kilio cha hofu sauti ya kutisha wala si ya amani.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

“Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Kumesikika kilio cha hofu sauti ya kutisha wala si ya amani.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

“Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Kumesikika kilio cha hofu sauti ya kutisha wala si ya amani.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

“Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “ ‘Vilio vya woga vinasikika: hofu kuu, wala si amani.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

“Hili ndilo asemalo bwana: “ ‘Vilio vya woga vinasikika: hofu kuu, wala si amani.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Maana BWANA asema hivi, Tumesikia sauti ya tetemeko, na ya hofu, wala si ya amani.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Yeremia 30:5
22 Marejeleo ya Msalaba  

Nao watanguruma juu yao siku hiyo Kama ngurumo ya bahari; Na mtu akiitazama nchi, ataona giza na dhiki Nayo nuru imetiwa giza katika mawingu yake.


Sisi sote twanguruma kama dubu; twaomboleza kama hua; twatazamia hukumu ya haki, lakini hapana; na wokovu, lakini u mbali nasi.


Watekao nyara wamepanda juu ya vilele vya milima katika nyika; kwa maana upanga wa BWANA utaangamiza toka upande mmoja wa nchi hata upande wa pili wa nchi; hapana mwenye mwili atakayekuwa na amani.


Sauti ya kilio cha wachungaji, na sauti ya kuomboleza kwao walio hodari katika kundi, kwa maana BWANA anayaharibu malisho yao.


Na haya ndiyo maneno aliyosema BWANA, kuhusu Israeli, na kuhusu Yuda.


Nimeyaona haya kwa sababu gani? Wamefadhaika, wamerudi nyuma; mashujaa wao wamevunjikavunjika; wanakimbia upesi sana, hawatazami nyuma; hofu iko pande zote; asema BWANA.


BWANA asema hivi, Tazama, watu wanakuja, wakitoka katika nchi ya kaskazini; na taifa kubwa litaamshwa, litokalo katika pande za mwisho wa dunia.


Ee binti wa watu wangu, ujivike nguo ya magunia, na kugaagaa katika majivu; fanya maombolezo, kama maombolezo kwa ajili ya mwana wa pekee, maombolezo ya uchungu mwingi; maana mwenye kuteka nyara atakuja juu yetu ghafla.


Kutoka Dani kumesikiwa mkoromo wa farasi wake; nchi yote pia inatetemeka kwa sauti ya mlio wa farasi wake wa vita; maana wamekuja, wamekula nchi na vyote vilivyomo; huo mji na wote wakaao ndani yake.


Tazama, sauti ya kilio cha binti ya watu wangu, itokayo katika nchi iliyo mbali sana; Je! BWANA hayumo katika Sayuni? Mfalme wake hayumo ndani yake? Mbona wamenikasirisha kwa sanamu zao walizochonga, na kwa ubatili wa kigeni?


Maana sauti ya maombolezo imesikiwa toka Sayuni, Jinsi tulivyotekwa! tulivyofadhaika sana! Kwa sababu tumeiacha nchi, kwa kuwa wameangusha makao yetu.


Nami nitazigeuza sikukuu zenu kuwa maombolezo, na nyimbo zenu zote kuwa vilio; nami nitatia nguo za magunia katika viuno vyote, na upara katika kila kichwa; nami nitayafanya haya kuwa kama maombolezo kwa ajili ya mwana wa pekee, na mwisho wake kama siku ya uchungu.


Naam, huwadhihaki wafalme, na wakuu ni kitu cha kudharauliwa kwake; huidharau kila ngome; kwa maana huirundikia udongo, na kuitwaa.


Kwa maana, angalieni, nawachochea Wakaldayo, taifa lile kali, lenye haraka kupita kiasi; wapitao katikati ya dunia, ili wayamiliki makao yasiyo yao.