Kabla ya masufuria yenu kupata moto wa miiba, Ataipeperusha kama chamchela, Iliyo mibichi na iliyo moto.
Yeremia 30:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tazama, tufani ya BWANA, yaani, ghadhabu yake, imetokea tufani ya kudumu; itawaangukia waovu vichwani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tazama, dhoruba kali kutoka kwa Mwenyezi-Mungu! Ghadhabu imezuka, kimbunga cha tufani kitamlipukia mtu mwovu kichwani. Biblia Habari Njema - BHND Tazama, dhoruba kali kutoka kwa Mwenyezi-Mungu! Ghadhabu imezuka, kimbunga cha tufani kitamlipukia mtu mwovu kichwani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tazama, dhoruba kali kutoka kwa Mwenyezi-Mungu! Ghadhabu imezuka, kimbunga cha tufani kitamlipukia mtu mwovu kichwani. Neno: Bibilia Takatifu Tazama, tufani ya Mwenyezi Mungu italipuka kwa ghadhabu, upepo wa kisulisuli uendao kasi utashuka juu ya vichwa vya waovu. Neno: Maandiko Matakatifu Tazama, tufani ya bwana italipuka kwa ghadhabu, upepo wa kisulisuli uendao kasi utashuka juu ya vichwa vya waovu. BIBLIA KISWAHILI Tazama, tufani ya BWANA, yaani, ghadhabu yake, imetokea tufani ya kudumu; itawaangukia waovu vichwani. |
Kabla ya masufuria yenu kupata moto wa miiba, Ataipeperusha kama chamchela, Iliyo mibichi na iliyo moto.
Hofu yenu ifikapo kama tufani, Na msiba wenu ufikapo kama kisulisuli, Dhiki na taabu zitakapowafikia.
BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, uovu utatokea toka taifa hata taifa, na tufani kuu itainuliwa toka pande za mwisho wa dunia.
Wakati ule watu hawa na Yerusalemu wataambiwa neno hili, Upepo wa moto utokao katika vilele vya nyikani visivyo na miti, ukimwelekea binti ya watu wangu, hauwi upepo wa kupepeta, wala upepo wa kutakasa;
Je! Si kitu kwenu, enyi nyote mpitao njia, Angalieni, mtazame Kama kuna majonzi yoyote mfano wa majonzi yangu, Niliyotendwa mimi, Ambayo BWANA amenihuzunisha kwa hayo Siku ya hasira yake iwakayo.
Naye BWANA ataonekana juu yao, Na mshale wake utatoka kama umeme; Na Bwana MUNGU ataipiga tarumbeta, Naye atakwenda kwa pepo za kisulisuli za kusini.