Yeremia 28:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi nabii Hanania akafa, mwaka uo huo, mwezi wa saba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwaka huohuo, mnamo mwezi wa saba, nabii Hanania akafa. Biblia Habari Njema - BHND Mwaka huohuo, mnamo mwezi wa saba, nabii Hanania akafa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwaka huohuo, mnamo mwezi wa saba, nabii Hanania akafa. Neno: Bibilia Takatifu Katika mwezi wa saba wa mwaka ule ule, nabii Hanania akafa. Neno: Maandiko Matakatifu Katika mwezi wa saba wa mwaka ule ule, nabii Hanania akafa. BIBLIA KISWAHILI Basi nabii Hanania akafa, mwaka huo huo, mwezi wa saba. |
Tazama, mimi niko juu ya manabii, asema BWANA, wanaotumia ndimi zao na kusema, Yeye asema,
Ikawa, katika mwaka ule ule, mwanzo wa kutawala kwake Sedekia, mfalme wa Yuda, mwaka wa nne, mwezi wa tano, Hanania, mwana wa Azuri, nabii, wa Gibeoni, akasema nami ndani ya nyumba ya BWANA, mbele ya makuhani na watu wote, akisema,
Basi BWANA asema hivi, Tazama, nakutuma uende zako toka juu ya uso wa nchi; mwaka huu utakufa, kwa sababu umenena maneno ya uasi juu ya BWANA.
Maneno haya ndiyo maneno ya barua, ambayo nabii Yeremia alituma toka Yerusalemu, kwa hao waliobaki wa wakuu waliochukuliwa mateka, na kwa makuhani, na kwa manabii, na kwa watu wote, ambao Nebukadneza aliwachukua mateka toka Yerusalemu hadi Babeli;
Lakini maneno yangu, na amri zangu nilizowaagiza hao manabii, watumishi wangu, je, Hazikuwapata baba zenu? Nao wakatubu na kusema, BWANA wa majeshi ametutenda kulingana na njia zetu, na matendo yetu, kama alivyokusudia kutenda.
Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa.