Basi kama baba yangu aliwatwika kongwa zito, mimi nitaongeza kongwa lenu; baba yangu aliwapiga kwa mijeledi, lakini mimi nitawapiga kwa nge.
Yeremia 28:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nenda ukamwambie Hanania, ukisema, BWANA asema hivi, Umezivunja nira za mti; lakini badala yake utafanya nira za chuma. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Nenda ukamwambie Hanania kwamba mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Wewe umevunja nira ya mti, lakini mimi nitatengeneza nyingine ya chuma. Biblia Habari Njema - BHND “Nenda ukamwambie Hanania kwamba mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Wewe umevunja nira ya mti, lakini mimi nitatengeneza nyingine ya chuma. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Nenda ukamwambie Hanania kwamba mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Wewe umevunja nira ya mti, lakini mimi nitatengeneza nyingine ya chuma. Neno: Bibilia Takatifu “Nenda ukamwambie Hanania, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Umevunja nira ya mti, lakini badala yake utapata nira ya chuma. Neno: Maandiko Matakatifu “Nenda ukamwambie Hanania, ‘Hili ndilo asemalo bwana: Umevunja nira ya mti, lakini badala yake utapata nira ya chuma. BIBLIA KISWAHILI Nenda ukamwambie Hanania, ukisema, BWANA asema hivi, Umezivunja nira za mti; lakini badala yake utafanya nira za chuma. |
Basi kama baba yangu aliwatwika kongwa zito, mimi nitaongeza kongwa lenu; baba yangu aliwapiga kwa mijeledi, lakini mimi nitawapiga kwa nge.
Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukatakata mapingo ya chuma;
Kwa maana mimi sikuwatuma, asema BWANA, bali wanatabiri uongo kwa jina langu; nipate kuwatoeni nje, mkaangamie, ninyi, na manabii hao wanaowatabiria.
Kongwa la makosa yangu limefungwa na mkono wake; Hayo yameshikamana; Yamepanda juu shingoni mwangu; Amezikomesha nguvu zangu;
Manabii wako wameona maono kwa ajili yako Ya ubatili na upumbavu Wala hawakufunua uovu wako, Wapate kurudisha kufungwa kwako; Bali wameona mabashiri ya ubatili kwa ajili yako Na sababu za kuhamishwa.
Huko Tapanesi nako mchana utakuwa giza, nitakapovunja huko kongwa za Misri, na kiburi cha uwezo wake kitakoma ndani yake, na katika habari zake, wingu litaifunika, na binti zake watakwenda utumwani.
kwa hiyo utawatumikia adui zako atakaowaleta BWANA juu yako, kwa njaa, na kwa kiu, na kwa uchi, na kwa uhitaji wa vitu vyote; naye atakuvika kongwa la chuma shingoni mwako, hata atakapokwisha kukuangamiza.