Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Yeremia 26:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Nawe utawaambia, BWANA asema hivi, Kama hamtaki kunisikia, kwenda katika sheria yangu, niliyoiweka mbele yenu,

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

“Utawaambia hivi: Mwenyezi-Mungu asema hivi: Msiponisikiliza na kufuata sheria zangu nilizowawekea,

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

“Utawaambia hivi: Mwenyezi-Mungu asema hivi: Msiponisikiliza na kufuata sheria zangu nilizowawekea,

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

“Utawaambia hivi: Mwenyezi-Mungu asema hivi: Msiponisikiliza na kufuata sheria zangu nilizowawekea,

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Waambie, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Ikiwa hamtanisikiliza na kuifuata sheria yangu niliyoiweka mbele yenu,

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Waambie, ‘Hili ndilo asemalo bwana: Ikiwa hamtanisikiliza na kuifuata sheria yangu ambayo nimeiweka mbele yenu,

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Nawe utawaambia, BWANA asema hivi, Kama hamtaki kunisikia, kwenda katika sheria yangu, niliyoiweka mbele yenu,

Tazama sura
Tafsiri zingine



Yeremia 26:4
22 Marejeleo ya Msalaba  

Bali mkighairi, mkaacha kunifuata, ninyi na watoto wenu, msizishike sheria zangu na amri zangu, nilizoziweka mbele yenu, tena mkienda na kuitumikia miungu mingine na kuiabudu,


bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha BWANA kimenena haya.


Lakini kama hamtaki kunisikiliza, kuitakasa siku ya sabato, kutokuchukua mzigo katika malango ya Yerusalemu siku ya sabato; basi, nitawasha moto malangoni mwake, nao utaziteketeza nyumba za enzi za Yerusalemu, wala hautazimika.


Lakini kama hamtaki kusikia maneno haya, mimi naapa kwa nafsi yangu, asema BWANA, ya kuwa nyumba hii itakuwa ukiwa.


nao wakaingia, wakaimiliki; lakini hawakuitii sauti yako, wala hawakuenda katika sheria yako; hawakutenda neno lolote katika haya uliyowaagiza wayatende; basi, kwa sababu hii umeleta juu yao mabaya haya yote;


Hawajanyenyekea hata leo, wala hawakuogopa, wala hawakuenenda katika sheria yangu, wala katika amri zangu, nilizoweka mbele yenu, na mbele ya baba zenu.


Kwa sababu mmefukiza uvumba, na kwa sababu mmetenda dhambi juu ya BWANA, wala hamkuitii sauti ya BWANA, wala hamkwenda katika torati yake, wala katika amri zake, wala katika shuhuda yake; ndiyo maana mabaya haya yamewapata kama ilivyo leo.


basi, nitaitenda nyumba hii, iitwayo kwa jina langu, mnayoitumainia, na mahali hapa nilipowapa ninyi na baba zenu, kama nilivyopatenda Shilo.


Nanyi angalieni mzifanye amri na hukumu zote niwawekeazo leo mbele yenu.


Kwa kuwa nitakapokwisha kuwatia katika nchi niliyowaapia baba zao, imiminikayo maziwa na asali; nao watakapokwisha kula na kushiba, na kuwanda; ndipo watakapoigeukia hiyo miungu mingine, na kuitumikia, na kunidharau mimi, na kulivunja agano langu.


Na torati Musa aliyowawekea wana wa Israeli ni hii;


Tena liko taifa gani kubwa, lililo na amri na hukumu zenye haki kama torati hii yote, ninayoiweka mbele yenu leo?


ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;